RASIMU YA KATIBA MPYA HADHARANI, WATANZANIA 1,015,564 WALITOA MAONI YAO


Kiu ya watanzania itakoma hii leo, ambapo rasimu ya katiba mpya imezinduliwa katika viwanja vya Karimjee jijini Da rs es Salaam na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kwenye tukio la kihistoria ambalo ndio muongozo wa kusongambele kwa taifa letu

Pamoja na hatua mbalimbali ambazo tume imezifanya kupata maoni hayo, lakini Maoni hayo yalitolewa na wananchi wapatao 1,015,564 kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na waliohudhuria mikutano ya moja kwa moja, waliotuma ujumbe mfupi wa simu (sms), barua pepe na kutumia mitandao ya kijamii.


Huku Idadi ya makundi yaliyotoa maoni ni 170 zikiwamo asasi 22 za kidini, 72 za kiraia, taasisi za Serikali 71, vyama vya siasa 19, viongozi na watu mashuhuri 43 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Rasimu hiyo ndiyo itakayopelekwa kwenye Mabaraza ya Katiba na itajadiliwa miezi mitatu ili kuona kama mapendekezo ya Tume hiyo baada ya kuchambua maoni hayo ya wananchi yanafaa au yanahitaji marekebisho. baada ya hayo yaliyojiri katika rasimu hiyo na mambo yaliyokuwa yakipigiwa kelele sana, majibu haya hapa.


TANZANIA SASA KUWA NA SERIKALI TATU

Muungano wa Tanzania na Zanzibar ulipigiwa kura nyingi ili iweze kuvunjwa na isiingie  katika Katiba mpya, Mwenyekiti wa mabadiliko ya Katiba Mpya Jaji Joseph Warioba amesema kutakuwa na Serikali tatu badala ya Serikali mbili za sasa.
Akitangaza rasmi ya katiba mpya Jaji Warioba alisema kwamba wameamua kuweka serikali tatu badala la serikali mbili za sasa. "Tumependekeza kuwa na serikali tatu badala ya serikali mbili na serikali hizo zitakuwa ni serikali Shirikisho,Serikali ya Bara pamoja na Serikali ya Zanzibar,tumezingatia uzuri na ubaya wa kuvunja muungano na kutazingatia changamoto za serikali tatu"
"Baada ya kuzingatia mambo hayo tukaona ni vyema tuwe na serikali tatu kwani watanzania wanaweza kuhimili changamoto zake kulika hasara ambayo itapatikana kwa pande zote mbili endapo tutaamua kuvunja muungano".

SASA RAIS KUSHITAKIWA
Jaji Joseph Warioba amesema kwamba itakuwa uhuru kwa kumshitaki Rais wa Serikali ya Shirikisho la Tanzania  Mahakamani na wagombea wa nafasi ya Urais endepo watagundua kwamba ushindi wake umejaa mashaka ya aina yoyote na kwamba kinga itakayoendelea kumlinda Rais ni ile ya kutokushtakiwa na mtu yoyote kuhusu masuala ya uchaguzi isipokuwa wagombea wa urais

"Imependekezwa kwamba matokeo ya kura za  urais  yatashtakiwa mahakamani lakini kwa masharti," alisema Jaji Warioba . Jaji Warioba ametaja masharti hayo kuwa ni pamoja na wagombea wa urais ndio watakuwa na haki ya kuhoji matokeo ya rais na si vinginevyo na kwamba matokeo hayo yanatakiwa kujadiliwa na kupingwa na wagombeo hao ndani ya mwezi mmoja tu na si vinginevyo.

SPIKA, NAIBU SPIKA HATATOKA CHAMA CHOCHOTE

NAFASI ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na naibu wake imefutwa katika Katipa Mpya ijayo badala yake Spika wa Bunge na Naibu wake hawataruhusiwa kuwa wa bunge wala mwanachama wa Chama chochote.

Hayo ni katika mapendekezo ya rasimu ya Katiba Mpya iliyotangazwa hivi punde katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba Mpya Jaji Joseph Warioba huku pia ikimpunguzia Rais Madaraka ya kuteuwa viongozi wa juu wa ngazi ya Serikali.

Tume hiyo pia imefanikiwa kufanya kazi iliyokuwa ikitarajiwa na wananchi hasa baada ya kujibu maswali mengi ya watanzania kuhusu muundao wa Serikali pamoja na masuala ya muungan

VITI MAALUMU KUJAZWA NA WALEMAVU

HATIMAYE watanzania wamepata suluhisho la matatizo yao baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Jaji mstaafu Joseph Warioba kutangaza mapendekezo ya katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi wenyewe.

Jaji Warioba alisema kwamba wamezingatia masuala mbalibali wakati wa kupitia na kuchambua maoni ya wananchi.
Kati ya mambo ambayo wananchi walikuwa wakiyapigia kelele ni suala la wabunge wa viti maalum ambayo Jaji Warioba alisema kwamba haitakuwepo katika katiba mpya badala yake nafsi hiyo itachukuliwa na kundi la watu wanye ulemavu ambao watakuwa wawili kutoka katika jimbo la uchaguzi.

Katiba ziliwahi kutengenezwa mwaka 1961 wakati Tanganyika ilipopata Uhuru, mwaka 1962 baada ya nchi kuwa Jamhuri, mwaka 1964 ilipoundwa Katiba ya Muda baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana na mwaka 1965 ilitungwa Katika Mpya iliyodumu hadi mwaka 1977 baada ya vyama vya Tanu na ASP kuungana na kuifanya nchi kuwa chini ya utawala wa chama kimoja cha siasa. Kwa upande wa Zanzibar kumekuwapo Katiba Tatu. Kwanza ni ile ya Uhuru iliyotungwa mwaka 1963, Mwaka 1979 ikatungwa Katiba nyingine na ya mwisho ni ile ya mwaka 1984.


EmoticonEmoticon