MASHINDANO YA MISS TEMEKE YAIVA, MSHINDI KUJULIKANA JULAI 5



MREMBO atakayetwaa taji la Redds Miss Temeke 2013, linalofanyika Ijumaa Julai 5, mwaka huu ataondoka na zawadi za jumla ya Sh. Milioni 3,250,000 ikiwa ni zawadi kubwa zaidi kutolewa katika mashindano yote ya urembo, yaliyofanyika mwaka huu.

Mshindi huyo, atapata ofa ya mwaka mzima kutoka RIO gym & Spa, iliyopo Quality Center, kutumia vifaa vyote ndani ya gym hiyo ambayo gharama yake ni Milioni 1,400,000, pia atajinyakulia simu ya kiganjani yenye thamani ya Sh 700,000 , dinner set kutoka AKO Catering yenye thamani ya Sh,150,000 sanjari na pesa taslim Sh. Milioni 1, hiyo jumla yake ni Milioni 3,250,000.

Mshindi wa pili katika mashindano hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abas Mtemvu atamkabidhi mshindi wa taji hilo kitita cha Sh.800,000 pamoja na dinner set ambayo thamani yake ilikuwa bado haijathibitishwa na mdhamni wa zawadi hiyo wakati mshindi wa tatu ambao wote kwa pamoja ni wawakilishi wa Miss Temeke, yeye atajipatia fedha taslimu Sh 700,000.

Sh , 400,000 zitakwenda kwa mshindi wa nne na atakayeshika nafasi ya tano yeye ataibuka na Sh 300,000. Washiriki wengine ambao hawatabahatika kuingia katika nafasi ya tano bora, wote watapewa Sh,200,000 kwa maana ya kifuta jasho. Tumelenga zawadi za fedha zaidi, hii ni kutokana na ugumu wa maandalizi kwa warembo ambao hugharamika zaidi, kiasi nasi kuona kuna kila namna ya kuwapunguzia maamivu hayo.

Shindano hilo, linatarajiwa kuwa na burudani ya kipekee kutoka kwa mshindi wa tungo bora ya Bongo Fleva ya Kili Music mwaka huu, Ben Paul sanjari na Twanga Pepeta ambayo mwishoni mwa wiki, ilizindua albamu yake ya 13 kwa mafanikio makubwa.

Warembo watakaopanda jukwaani Julai 5 ni kutoka Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambao wanawania taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba tatu, Edda Sylvester walikuwa chini ya wakufunzi Suzy Mwenda na Shadya Mohamed 

Warembo hao ni pamoja na Axsaritha Vedastus, Darling Mmary, Esther Muswa,  Hyness Oscar, Irene Rajab, Jamila Thomas, Latifa Mohamed, Margreth Gerald, Margreth Olotu, Mey Karume, Mutesi George, Naima Ramadhan, Narietha Boniface , Stella Mngazija na Svtlona Nyameyo .                                                                 


EmoticonEmoticon