BARABARA ZIJENGWE USIKU NA MCHANA, WANAO KAIDI KUPISHA UJENZI KUKUMBANA NA SHERIA ASEMA MAGUFULI

Pichani ni Mhe. John Magufuli akiangalia kipimo cha lami katika barabara ya Magomeni (Magari yaendayo kasi)


Waziri wa ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli leo hii ametembelea barabara zote zinazoendelea kujengwa katika jiji la Dar es salaam, akifanya ukaguzi wa miradi hiyo Magufuli amewataka wakandarasi wanao simamia barabara hizo kujenga usiku na mchana ilikuweza kumaliza kazi zao kwa wakati kulingana na mikataba yao

“Akiongea na waandishi wa habari katika ziara hiyo Mhe. Magufuli amesema kuwa matatizo madogo madogo yasi kwa mishe kazi hivyo wafanye kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa kazi zao zinamalizika kwa wakati na kiwango kinacho takiwa” Amesema

Magufuli amesema kuwa hata katika nchi zilizoendelea kazi ya ujenzi hufanyika usiku na mchana hivyo wakati wa usiku nivyema zaidi kwani msongamano wa magari huwa yamepungua.

Aidha Magufuli amewataka wakazi wa Dar es salaam kutambua kuwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya bara bara katika jiji hilo ni kutatua tatizo la msongamano wa magari ilikuweza kuwezesha usafiri wa haraka zaidi.

“Wakazi wa Dar es salaam wamekuwa wakilalamika sana juu ya ujenzi unaoendelea kila mahali kutokana na barabara nyingi kutumika wakati zinajengwa, wengine wanakataa kupisha barabra wakati maendeleo ni yetu wote”Amesema


Wale ambao wamekataa kupisha ujenzi wa barabara wajenge tuu juu ya barabara alafu ujenzi utawakuta hapo, na hili halina kulazimisha sana kwa mtu anaye vunja sheria nakama mtu analalamika aende mahakamani. Amesema

Magufuli amesema kwa barabara ambazo ziko chini ya kiwango wakandarasi wanao husika watalazimika kuanza upya ujenzi huo pamoja na kutumia fedha zao kumalizia kazi ambayo hayaija kamilika

Katika ziara hiyo Magufuli ametembelea barabara zote zinazo endelea kujengwa jijini Dar es salaam moja wapo zikiwa ni barabara ya kutoka Mwenge mpaka Tegeta, Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, Ujenzi wa Mradi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi kutokea kimara hadi Posta pamoja na ujenzi wa barabara ya Kilwa.


EmoticonEmoticon