AMIRI JESHI MKUU RAIS JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA MAMIA KUAGA MIILI YA WANAJESHI 7 WA TANZANIA WALIOUWAWA DARFUR


Rais wa Tanzania Jakaya Kiwete amewaongoza maelfu ya waombolezaji katika kutoa heshima zao za mwisho kwa wanajeshi saba wa Tanzania waliouawa kwa kushambuliwa na waasi Darfur nchini Sudan walipokuwa wakilinda amani.


Rais Kikwete amesema nchi ya Sudana ifanye uchunguzi wa haraka juu ya vifo vya wanajeshi hao ili kubaini ni kina nani wamehusika katika shambulio hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa” Alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa Wanajeshi wetu walienda kuwalinda ili waweze kuwa na amani katika nchi yao na sivinginevyo. Alisema




Miili ya wanajeshi hao iliwasili jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi, na kupokelewa na mamia ya waombolezaji walioongozwa na makamu wa rais Dokta Gharib Bilal, katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya kijeshi ya Lugalo.

Zoezi la kuwaaga wanajeshi hao imefanyika katika uwanja wa makao makuu ya jeshi eneo la Upanga jijini DSM, ambapo wanajeshi wawili kati yao watasafirishwa visiwavi Zanzibar kwa mazishi


Wanajeshi hao ni pamoja na Sajenti Shaibu Shehe, Corporal Oswald Chaulo, Corporal Mohammed Ally, Corporal Mohammed Chukilizo, Private Rodney Ndunguru, Private Fortunatus Msofe na Private Peter Werema.

Rais wa Sudan Omar Al Bashir alimhakikishia Rais Jakaya Kikwete kuwa wote waliohusika katika kuwashambulia wanajeshi hao na kuwaua watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Rais Bashir alitoa ahadi hiyo wakati wa mazungumzo na Rais Kikwete na kuongeza kuwa anaamini waliohusika na mauaji hayo walikuwa wahalifu na kuwa lazima wasakwe.


EmoticonEmoticon