CCM YA BURUZWA NA CHADEMA ARUSHA, WASHINDA KATA ZOTE VIONGOZI WA DINI NAO WAPONGEZA UTULIVU ULIOPO




Viongozi wa Madhebu ya Kidini mkoani Arusha wameeleza kuridhishwa na hali ya amani iliyotawala katika uchaguzi mdogo wa Madiwani katika kata za Jiji la Arusha na kuzisifu vyombo vya dola pamoja na wananchi kwa kudumisha amani na kuepuka vurugu zisizo za lazima.

Habari zilizo ifikia Blog hii toka mkoani humo zinasema, Viongozi wa kidini Wakizungumzia hali hiyo, kutoka katika madhehebu tofauti wamesema, amani itaendelea kuwepo kwani utulivu ulioonyeshwa na vyombo vya dola pamoja na wakazi wa Arusha unapaswa kuendelea katika chaguzi zijazo.

Naye Mkurugenzi wa kituo cha Taarifa kwa wananchi Deus Kibamba amesema watendaji wa serikali wakiweza kusimamia demokrasia kwa kiwango hicho, hakuna vurugu wala umwagaji wa damu utakaotokea hapa nchini.

Kwa upande mwingine, Wanachama wa Chama cha Mapindizi wamewataka viongozi wa Chama hicho kwa Wilaya ya Arusa kujithamini kutokana na anguko walilolipata katika Uchaguzi huo, ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeshinda katika kata zote nne.

Chama cha Chadema kimethibitisha ushindi wake baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye mkoa huo, Uchaguzi huo ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na ulikuwa unachukuliwa kama kipimo cha siasa komavu mkoani humo
Chadema kimeongoza katika vituo vyote136 vya kupigia kura katika Kata za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi.
Matokeo hayo yameonyeshwa kulingana na idadi ya vituo katika kata mbali mbali ambapo Matokeo ya Uchaguzi katika kata hizo nne na vituo 136 yalikuwa kama ifuatavyo:
Kata ya Elerai CHADEMA kura 2,047  CCM kura 1,471
Kata ya Themi CHADEMA kura 674 CCM kura 326
Kata ya Kaloleni CHADEMA kura 1,470 CCM kura 330
Kata ya Kimandolu CHADEMA kura 2,761 CCM kura 1,163


Baadhi ya Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya Chadema kuwatimua wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih Mallah(Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni


EmoticonEmoticon