Picha ya mtoto aliye zikwa akiwa hai mbeya na baba yake, hapo ni baada ya kufukuliwa na polisi |
Haki ya kuishi kwa
watanzania imeendelea kukiukwa katika kipindi cha miezi sita
iliyopita kupitia matukio mbalimbali yaliyo kinyume na haki za
binadamu ikiwa ni pamoja na Polisi kuua raia, polisi kuuawa mikononi
mwa raia, mauaji ya alibino, mauaji ya vikongwe kwa imani za
kishirikina, wananchi kuvamia vituo vya polisi, vitendo vya ubakaji.
Hayo yameelezwa katika
taarifa ya hali ya haki za binadamu nchini katika kipindi cha kuanzia
January hadi June mwaka huu iliyotolewa leo na kituo
cha sheria na haki za binadamu ambayo pia inaonesha kuongezeka kwa
vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vitendo ambavyo vinatokana
na wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Mtafiti kutoka kituo
hicho Bwana Pasience Mlowe ndiye aliyesoma taarifa hiyo mbele
ya waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam ambapo amesema
kuwa elimu ya kutosha juu ya haki za binadamu itolewe kwa wananchi
ili kuzuia vifo visivyo vya lazima hapa nchini
Katika kipindi cha
January hadi june mwaka huu Jumla ya askari polisi 8 wameuawa
na wananchi, raia 22 wameuawa chini ya vyombo vya ulinzi,
watoto 127 wametupwa, watoto 394 wamelatiwa, vifo 597
vimetokana na raia kujichukulia sheria mkononi, vifo 303
vimetokana na imani ya kishirikina na vitendo 2965 vya
ubakaji vimeripotiwa.
Katika matukio ya kubakwa
huko ukerewe mwanza mwanaume wa miaka 40 aliyejulikana kwa jina la
Emanuel Halala alimbaka mara mbili mtoto wa miaka 8, huku mtoto wa
miaka 3 aliye bakwa na mwanaume wa miaka 30 huko mkoani Mbeya matukio
ambayo yanazidi kila ripo zinavyo zidi kutolewa
Aidha kuna mtoto aliye
zikwa akiwa hai na baba yake huko Mkoani Mbeya kwa madai ya kuachana
na mama yake mtoto huyo alikuwa wa miaka 4, lakini katika matukio
mengi hakuna hatua zozote za kisheria zilizo chukuliwa didhi ya
wahusiaka wa matukio hayo.
Shirika hili limeitaka serikali kuendesha kampeni juu ya elimu ya haki za binadamu kama ambavyo wamefaulu katika maleria na ukimwi ilikuondoa matendo ya ukatili na unyanyasaji katika jamii ya watanzania.
EmoticonEmoticon