"OBAMA LEAVE HOPE" UMEME AJIRA KWA VIJANA TANZANIA


Watanzania asilimia 70% ambao hawajafikiwa na umeme huwenda wakasahau giza mara baada ya Rais wa Marekani bwana Barack Obama kutembelea hapa nchini kwa ziara ya siku mbili.

Akizindua mradi mkubwa wa umeme katika kituo cha kufua umeme cha Ubungo ambapo Mitambo ya Symbion inapatikana Rais Obama amesema Marekani itawezesha upatikanaji wa umeme kwa kila mtanzania akiwa katika makazi yake au nyumbani kwake.

“Tutawezesha kuwepo kwa umeme wa uhakika angalau kila mtanzania aweze kutumia umeme katika kila shugulizake na anapo kuwa nyumbani ilikuweza kupata maendeleo ya haraka na kukuza uchumi” Alisema Obama.


Obama alisisitiza kuwa “African countries should be Donors, not to receive all the time” Ni lazima waafrika wawe wawezeshaji wao wenyewe na sio kuwa wapokeaji kila wakati. Alisema.

Serikali ya Marekani imetoa Dola Bilioni 7, huku Dola Bilioni 9 zikipatikana kutoka katika sekta binafsi nchini humo ili kuweza kutekeleza mpango wa umeme kwa nchi za Afrika.


Pia Marekani itaisaidia Tanzania katika vipaumbele vya Umeme wa uhakika, Miundo mbinu ya barabara, Maji, Elimu na kuwainua Vijana ambapo kila mwaka kutakuwa na vijana kadhaa watakao hudhuria masomo nchini marekani.

Kwa sasa Tanzania  inazalisha megawati 1438.24 ikiwa na malengo ya kuzalisha megawati 2780 mpaka 3000 ifikapo mwaka 2015.
Naye  Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Prof Sospeter Muhongo ameeleza kuwa mpango huu umekuja wakati muafa ambao utasaidia miradi mikubwa ya umeme kuendelea hapa nchini.
“Sera ya marekani ya kufikisha umeme itapunguza umasikini na tumekuwa na neema miongoni mwa nchi chache zilizo baatika kupewa fursa hii”Alisema.
Mpango huo wa umeme utahusisha nchi 7 ambazo ni Tanzania, Kenya, Senegal, Msumbiji, Liberia, Ethiopia na Nigeria.


EmoticonEmoticon