DR. SLAA SIMTAMBUI TENDWA, ASEMA READ BRIGADE ILIANZA TANGU 2004



Katibu mkuu wa chama cha Democrasia na maendeleo Chadema Dr. Wibroad Slaa amesema kuwa chama hicho akimtambui msajili wa vyama vya siasa nchini Gaji John Tendwa na kwamba wamefuta kiasi kwamba hawashirikiani nae katika kazi zao.

Dr. Slaa amezidi kusema kuwa hawata shirikiana na  Tendwa mpaka atakapo ondoka madarakani lakini Dr. Slaa alisisitiza kuwa chama chake inaeshimu sana ofisis ya msajili wa vyama vya siasa na kutambua uwepo wake.

"Msajili wa vyama vya siasa anatakiwa kulea vyama vya siasa na sio kukandamiza upande mmoja, yeye hatungi sheria na taratibu zote tumefuata za kusajili chama, labda atuambie nikifungu gani atatumia kukifuta chama" Alisema Dr. Slaa.

Hayo yamekuja baada ya Dr. Slaa kufanya mahojiano na wanahabari alipokuwa kwenye ufunguzi wa kongamano la demokrasia lililo chini ya taasisi ya kimataifa ya inayojishugulisha na mambo ya kidemokrasia inayojulikana kama International Young Democrat Union IYDU.

Hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkali kati ya CHADEMA na ofisi ya msajili ambapo ofisi ya msajili ilikitaka chama hicho kuachana na mpango wake wa kuunda vikundi vya ulinzi na endapo kitakaidi atakifutia usajili chama hicho.

Kuusiana na suala la Read Brigade Dr. Slaa amesema kuwa chama chake hakikuanza mwaka huu, tangu mwaka 2004 chama hicho kilikuwa na kikundi hicho hivyo kama kuna sheria inawafunga kufanya hivyo wangependa kudhibitishiwa.

Aidha kuusiana na swala la amani Dr. Slaa amesema kuwa kama serikali ingeweza kutatua matatizo ya ardhi na kuondoa kero hasa za ubadhirifu wa fedha kwa viongozi amesema amani ipo ila nimuhimu kwa serikali kuweka mazingira ambayo yataondoa malalamiko miongoni mwa wananchi.

Hatahivyo Mwenyekiti wa Bavicha Mhe. John Heche amesema mkutano huo wa kuangalia masuala ya Demokrasia katika nchi mbali mbali duniani umeshirikisha nchi zaidi ya 18 ndani ya Afrika na nje ya Afrika.

Heche amesema, yeye ndiye Mjumbe wa bodi ya vijana ya Dunia hivyo wataitumia fursa hii kuleta mabadiliko kwa vijana katika ushirikiano wao kwenye siasa, fursa za ajira pamoja na uwezo wa kuzalisha ili kuweza kujiwezesha kiuchumi.

"Bila vijana kukombolewa taifa halita inuka kikubwa ni kufanya mabadiliko na kuwapa ewezo zaidi vijana na sisi tuna wataka wafanye mabadiliko na washiriki kikamilifu katika kufanya mabadiliko" amesema Heche

Baadhi ya nchi zilizoshiriki katika mkunao huo ni Germany, Italy, Spain, Finland, Kenya, Uganda, Togo na nchi zingine nyingi.

Hatahivyo Heche amesema, chama chake kita wasilisha matatizo yote wanayo kumbana nayo kutoka kwa vyombo vya dola kama kuzuiliwa mikutano yao ya kisiasa, ukatili kutoka kwa polisi dhidi ya raia, vifo katika mikutano yao mfano David Mwangosi na mengine mengi.

Lengo la kuwasilisha hayo nikuuambia ulimwengu yanayojiri hapa nchini. amesema Heche.


EmoticonEmoticon