VIJIJI 1000 TANZANIA VYA ANDALIWA KUONGEZA CHAKULA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI


Zaidi ya vijiji 1000 nchini Tanzania vinatarajiwa kupewa elimu ya kuhifadhi mazingira kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa chakula katika nchi za Afrika mashariki.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam katika warsha ya siku tatu, yenye nia ya kuwapa mbinu mpya wakulima, Mkurugenzi mkuu wa ESRF bwana Bohela Lunogelo amesema Tanzania ndiyo inaongoza kwa uzalishaji wa chakula katika nchi za ukanda huo hivyo ni muhimu kuanza kupata elimu hiyo.

“Nchi nyingi za afrika mashariki zinaitegemea Tanzania kwa chakula,

Warsha hiyo ya siku tatu iliyoandaliwa na taasisi inayojishughulisha na utafiti wa kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na taasisi zingine za kimataifa zinazojishugulisha na Mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya Kibiashara imeanza leo na inatarajiwa kumalizika tarehe Julai 10, ikiwa na majibu ya nini kifanyike ili kuweza kupata chakula cha kutosha kwa nchi za Afrika mashariki.


 MATUMIZI YA MAFUTA YA UBUYU NI HATARI KWA AFYA 

Mamlaka ya chakula na Dawa nchini TFDA, imetoa onyo kwa watumiaji wa mafuta ya ubuyu kwa kuwa mafuta hayo yana madhara kwa afya na kuwaasa wanao tumia mafuta hayo waache mara moja.

Akiongea na mtandao huu mapema leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa usalama wa chakula TFDA bwana Raymond Wigenge amesema, pamoja na mafuta hayo kuwa na madhara pia haiwezekani kwa kitu kinachotumika kama chakula kutumika kama dawa.

“Hakuna dawa iliyo wahi kutumika kama dawa na wakati huo huo ni chakula, madhara tuliyobaini ni mengi ila kansa yaweza kusababishwa na matumizi ya mafuta haya”amesema

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na matumizi ya mafuta ya Ubuyu yanayozalishwa zaidi mkoani Dodoma na wafanyabiashara wadogo wadogo wakidai kuwa mafuta hayo yanaweza kutumika kwa kupikia, dawa au vipodozi lakini TFDA inapinga vikali matumizi yake.


EmoticonEmoticon