WANAFUNZI EFU 33,683 KUJIUNGA KIDATO CHA TANO2013, 530 WAPELEKWA VYUO VYA UFUNDI, HUKU LAKI 397,437 WAKISOTA MTAANI



Jumla ya wanafunzi 34,213 sawa na asilimia 18.1 ya waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 kwa madaraja ya I – IV wamechaguliwa kuingia kidato cha tano na vyuo vya ufundi pamoja na taasisi ya menejiment ya maendeleo ya maji kwa mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 2,790 sawa na asilimia 8.9 ikilinganishwa na mwaka 2012.

Aidha Jumla ya wanafunzi 33,683 sawa na asilimia 18.1 ya waliofaulu wakiwemo wavulana 23,383 na wasichana 10,300 wamechaguliwa kuingia kidato cha tano kwa mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.15 ikilinganishwa na mwaka 2012.

Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe Philip Mulugo ndiye aliyetoa taarifa hiyo leo jijini DSM na kusema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa mwaka huu ni wa masomo (Tahasusi) ya Sayansi.

Mhe. Mulugo amesema wanafunzi wa some kwa bidii bila kujali aina ya masomo anayosoma, pamoja na kuwasisitiza wanafunzi wa kike kujiamini kuwa wanaweza masomo yote, Alisema

Idadi ya wanafunzi wote waliojiunga na vyuo vya ufundi imepungua kutoka 564 mwaka 2012 hadi 530 mwaka 2013 ambapo wavulana ni 416 wasichana wakiwa 114 tu. Lakini hilo niongezeko kubwa kwa upande wa wasichana ambao kwa mwaka huu wamechaguliwa 144 tofauti na mwaka jana ambao walikuwa 47 tu.

Kuhusiana na baadhi ya wanafunzi ambao tayari wame kwisha anza masomo ya kidato cha tano katika shule binafsi, Mhe Mulugo ametoa ufafanuzi kuwa shule za serikali hufunguliwa Julai ambapo waliochaguliwa watatakiwa kuripoti tarehe 29 Julai

Wanafunzi ambao tayari wameanza kusoma masomo ya kidato cha tano katika shule binafsi na wamefauli katika shule za serikali ni uamuzi wao kuamua kama waendelee na shule za binafsi au warudi kujiunga na shule za serikali ila wasiihusishe serikali” Amesema

Matokeo haya yanaonesha kuwa, shule za serikali zitakumbwa na upungufu wa wanafuzi takribani 10,097 wengi wao wakiwa ni wa masomo ya sanaa.

Kwa taarifa ya Waziri Jumla ya Wanafunzi Laki 397,437 hawacha chaguliwa kujiunga na masomo ya juu, na kati ya hawa kuna waliopata daraja la IV na 0 ambao ndio wengi kuliko waliochaguliwa


EmoticonEmoticon