Mchaka mchaka unaendelea kwa viongozi wa juu, vyombo vya
uasala pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na ujio wa marais wengi kwa
kipindi cha wiki mbili Mfululizo
Ikumbukwe hapo wiki jana kulikuwa na mkutano wa Smart
Pertnership International Dialogie 2013 hapa nchini mkutano ulijumuisha marais
wapatao 9, mkutano huo umemalizika hii leo jijini Dar es salaam
Hii leo tena tumeshuhudia ugeni mkubwa wa Barack Obama na
mkewe Michell Obama pamoja na Familia yeke, wakati huo huo hapo kesho tutapata
ugeni wa Rais mstaafu George W Bush pamoja na mkewe Bi Laura
Viongozi hao wa marekani hapo kesho watakuwa na shuguli
nyingi Obama akitakiwa kushiriki matukio 10 huku Michell na Laura wakiwa na
mazungumzo na Wake wa marais wa barabi Afrika na mwenyeji wao Mama Salma
Kikwete lengo ikiwa ni kuinua wanawake nchini
Katika matukio yatakayo hudhuriwa na Obama hapo kesho, ni Uzinduzi wa mpango wa Simbioni utakao fanyika
katika kituo kikuu cha kuzalishia umeme cha Ubungo, pia ataweka Shada la maua
katika ubalozi wa marekani ikiwa ni kumbukumbu ya watu waliouwawa katika
shambulizi la kigaidi la bomu mwaka 1988 huku Dar es salaam pamoja na kutembelea
kituo cha watoto wa mitaani.
Wananchi wanatakiwa kuamka asubuhi na mapema ili kuepuka
adha itakayo tokana na barabara kufungwa kwa muda ilikupisha shuguli zitakazo fanywa na
raisi huyo kumalizika kwa wakati
Barabara zitakazo fungwa ni Barabara ya Nyerere kuanzia saa
3 hadi saa 5 asubuhi, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Sam Nujoma na barabara ya
Morogoro, Nelson Mandela ambayo ataitumia wakati akiondoka hapo kesho kurejea
marekani
Ongeza kichwa |
EmoticonEmoticon