Serikali imetakiwa kuweka sheria za
majenzi ili kuweza kuwadhibiti na kuwachukulia hatua wanao kiuka taratibu za
kujenga kwani mpaka sasa hakuna sheria inayowatia hatiani hata pale inapotokea
jengo limebomoka na kusababisha madhara kwa jamii.
“Tume shuhudia
jengo lime bomoka hivi karibuni lakini ningumu kuchukua hatua za kisheria juu ya
wahusika kwakuwa sheria ya kuwatia hatia ahipo, hivyo serikali ilishugulikie
hili swala na tunaliomba Bunge kuangalia zaidi”amesema Hussein
Ameongea hayo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari
katika mkutano uliowakutanisha wasanifu majengo wa Afrika mashariki kwa lengo
la kujadili ni jinsi gani wataweza kutumia fedha zao kuendeleza vyuo vinavyotoa
taaluma ya majengo katika nchi za ukanda huo, Rais wa chama cha Wasanifu
majengo Tanzania Arch. Husein Igangula amesema watatumia fedha zao kuendeleza
taaluma hiyo.
“Tangu
Jumuiya hii ianzishwe nimiaka mingi sasa na tumeona kuwa fedha nyingi
tulizonazo benki zitumike kuendeleza vyuo vinavyo fundisha taaluma hiyo ikiwa
pamoja na wale wanafunzi wanao chukua somo hilo ilikuweza kupata wafanisi
zaidi”Amesema Hussein
Tunataka kulinda rasilimali zetu na fedha tulizo nazo, ilitupate
mbinu za kushindana na wachina ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanaotumiwa na
nchini mwetu katika kufanya ujenzi mbalimbali.
“Mbinu za
kushindana na wachina nipamoja na kuongeza ufanisi wetu kupitia elimu na
teknoligia za kisasa, na kwakweli hapa nchini kuna wasomi sio kwamba hawapo
kuwatumia wachina kila mara katika kazi ambazo hata wazawa wanaziweza ndicho
tunacho pambana nacho hivi sasa”amesema Hussein.
Aidha ameitaka serikali kuwatumia wazawa katika kazi zake
nakusisitiza kuwa kazi zaio zinagarimu pesa nyingi hivyo mianya ya rushwa
inaweza ikawepo hivyo watanzania pia waondokane na swala hilo ilikuweza
kuwainua wasanifu majengo wandani.
Naye Arch Kaisi Kalaamboambaye alikuwepo
kwa niaba ya Raisi wa Jumuhiya hiyo barani Afrika amesema ni vyema wananchi
wakajenga tabia ya kuwatumia wasanifu majengo katika ujenzi wao bila kuhofia
garama kwani wao wapo kwaajili ya watu wote.
“Wanaojenga
nyumba ndogo pia wanahitaji wasanifu wasihofie garama kwani kila garama ipo
kwaajili ya kazi husika, nyumba ikiwa ndogo garama pia nindogo hivyo
wasiogope”amesema Kaisi.
Mkutano huo wasikimbili umewakutanisha wasanifu majengo ukada wa
afrika mashariki na hutamalizika hapo kesho jijini Dar es salaam.
EmoticonEmoticon