MILLIONI MIA 320 KUOKOA WANAWAKE WAJAWAZITO, RUKWA NA MWANZA



Serikali imegundua njia mpya yakuwawezesha wanawake kuhudhuria hospitali wakati wakujifungua baada ya kubaini kuwa, Asilimia 98 ya wanawake wanahudhuria kliniki ni asilimia 51 tu kati yao ndio hurudi tena kujifungua katika vituo hivyo

Hayo yamesemwa na Mganga mkuu wa serikali Dr. Donan Mmbando wakati akipokea magari 4 ya wagonjwa yenye dhamani ya shilingi Millioni 32 kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na huduma za wazazi na mwana la Plan International, magari ambayo yatatumiwa mkoani Rukwa na Mwanza

Kushoto ni Mganga Mkuu wa serikali Dr. Donan Mmbando, katikati ni Mwakilishi wa CIDA Jonathan Arnold, kulia ni David Muthungu kurugenzi wa Plan International

“Idadi kubwa ya wanawake huripoti kliniki lakini wachache sana ndio hurudi kujifungua hospitalini, hii husababishwa na kukosa huduma za kijifungulia, fedha ya matibabu na maamuzi ya kifamilia pengine kutokana na umbali mrefu wa kupata huduma za afya” Alisema Dr Donan

Dr. Donan amesema, Tanzania inajitahidi iliiweze kufanikisha malengo ya Millenia ifikapo mwaka 2015 kwakupunguza vifo vya wanawake wakati wa kujifungua pamoja na vifo vya watoto wachanga baada ya kuzaliwa kutoka asilimia 32 mpaka asilimia 26 kwa watoto.




Vifo vingi vya wanawake hutokana na kutokwa damu nyingi kabla na baada ya kujifungua, Maleria na Anemia, pamoja na Virusi vya ukimwi, kujifungua katika umri mdogo pamoja na sababu nyingine nyingi , lakini kwa watoto wanafariki maratu wanapo zaliwa ni Elfu 45 ndani ya mwaka mmoja. Alisema Dr. Donan

Plan International imebaini kuwa katika mkoa wa Rukwa niasilimia 29 tu ya wanawake ndio huudhuria hospitali wakati wakujifungua wakati mkoani Mwanza ni asilimia 44. hii hutokana na umbali wa huduma za Afya kwa jamii za zijijini katika mikoa hiyo

“Tafiti za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya watanzania wanakaa kilometa 10 kutoka kilipo kituo cha Afya nahii inachangia kiwango cha juu cha kina mama kujifungua nyumbani” alisema Mkurugenzi wa Plan International bwana David Muthungu



Shirika hilo limetoa msaada wa magari 4 yenye dhamani dola 200,000 ambayo nisawa na shilingi Millioni miatatu na ishirini (320,000,000)  iliyaweze kutumika katika mikoa ya Rukwa na Mwanza ilikuwezesha wanawake kujifungua hospitali na kupunguza vifo wakati wakujifungua

Magari hayo yatawekwa katika vituo vya Afya ilikutoa huduma ya dharura kwa wajawazito na watoto wachanaga katika vituo vya Wampembe na Mtowisa vya Rukwa vijijini na Mwangika na Sangubuye vya Sengerema mwanza. Huku ikikadiriwa kuwa wanawake laki 3 watanufaika na msaada huo.


EmoticonEmoticon