Mashindano ya Dance yanayo fanywa na kituo cha utangazaji cha EATV yanayo kwenda kwa jina la DANCE 100% yameanza tena kwa kishindo huku makundi kibao yakijitokeza kuwania nafasi ya kushiriki mashindano hayo ambapo mshindi atajinyakulia pesa taslimu Millioni 5.
Katika kujiandikisha kwa awamu ya kwanza uliofanyika katika viwanja vya TCC Chang'ombe, jumla ya makundi 15 yalijitokeza siku hiyo ambapo makundi 5 tu ndio yalishinda kuingia katika mashindano hayo, Kumbuka mashindano haya yatarushwa hewani na kituo hicho kuanzia saa 1 jioni siku ya jumatano.
Makundi yaliyoshinda ni Ikulu Vegas, Ganzi More Fire, The Chocolate, D.D.I Crew na The W.T kati ya makundi 15 yaliyojitokeza uwanjani hapo
Makundi mengine yaliyoshiriki lakini hayakuibuka kidedea ni Mtwara Dancers, SMB, Black Winners, Moa Dancers, Wakali Popote, Waku shine, Black Texas, The new black, NB Ndala na Leo Tena,
Katika hamu hii Dance 100% haitachukua wakali wa Wilaya ilikuweza kuwapa nafasi kila kundi litakalo penda kushindana. Awamu ya pili itafanyika viwanja vya Don Bosco Oyster bay siku ya tarehe 30. 6. 2013 kuanzia hasubuhi.
Shindano hili linasimamiwa na majaji watatu ambao nao ni wataalamu wa ku Dance wakiongozwa na Lotus Kyamba, Supa Nyamwela na Adam Juma, huku ikisindikizwa na watangazai bora kabisaaa Saigon na Babs.
Dance 100% ya mwaka 2012 kundi la T Africa liliibuka kidedea na kujinyakulia kitita cha Millioni 5 kutoka EATV ambapo awamu hii mshindi atajinyakulia kiasi hichohicho cha Millioni 5. mashindano haya yanafanywa na kituo cha utangazaji cha EATV.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon