MATOKEO YA KIDATO CHA SITA, ASILIMIA 93 WAFAULU



Baraza la mitihani Tanzania, leo limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika mwezi February mwaka huu, huku asilimia 93.9 ya watahiniwa wamefaulu mtihani huo

Akitangaza matokeo hayo katika ofisi za baraza hilo Mikocheni jijini DSM, Naibu katibu mtendaji wa baraza hilo Dr Charles Msonde amesema Jumla ya watahiniwa 40,242 kati ya watahiniwa 42,952 wa shule, sawa na asilimia 93.92 wamefaulu kwa daraja la I hadi la IV

Matokeo haya yanaonesha kuwa kwa mwaka huu ufaulu kwa watahiniwa wa shule umeongezeka kwa takribani asilimia 1.6. wakati kwa matokeo ya jumla matokeo yamepanda kwa takriban asilimia 0.2. hapo mwaka 2012 watahiniwa Elfu 40,775 sawa na asilimia 92.30 ya watahiniwa walifaulu mitihani hiyo.

Aidha Dr msonde ametaja shule 10 bora, zilizoongozwa na Marian Girls ya Pwani katika kundi la watahiniwa zaidi ya 30, ikifuatiwa na Mzumbe sekondary school iliyopo Morogoro. Shule zilizo fanya vibaya Pia ametaja watahiniwa waliofanya vizuri katika masomo mbalimbali, 

Kwa upande wa Sayansi aliyeongoza ni Erasmi Inyanse aliyekuwa akisoma PCM kutoka shule ya Ilboru Arusha, kwa masomo ya biashara wa kwanza ni Erick Robert Mulogo kutoka Tusiime ya DSM kombi ya ECA, na kwa masomo ya lugha na sayansi ya Jamii kwa kwanza ni Asia Idd Mti kutoka Barbro-Johansson ya DSM alikuwa akisoma HGE

Aidha, Watahiniwa watano wa kiume bora kwa somo la Sayansi kuwa ni, Erasmi Inyanse kutoka Ilboru, Maige R Majuto kutoka shule ya Kisimiro, Gasper Singfrid mungongo wa Feza boys, wanafunzi wa kike walio fanya vizuri kwa somo la Sayansi ni Lucylight E Mallya wa Marian Girls, Edna Baraka Kibango wa Msalato na Sara Severin Kimario wa St. Marys mazinde juu.

Hatahiyo baraza la mitihani ilmezuia kutoa matokeo ya mitihani wa kidato cha sita kwa wanafunzi 89 kwa sababu za kutomaliza ada ya mitihani na matokeo yao yatatoka mpaka hapo watakapo lipia mitihani hiyo, 27 walipata matatizo ya kiafya hivyo watapewa fursa ya kurudia mitihani yao mwaka 2014


FUNGUA HAPA KUANGALIA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2013


EmoticonEmoticon