Chama
cha walimu Tanzania kimeitaka jamii kutambua kuwa mgogoro kati ya
walimu na serikali bado upo palepale kutokana na serikali kutokubali
kutekeleza madai ya walimu kwa kiwango wanachohitaji.
Akiongea
leo jijini Dar es salaam, Rais wa chama cha walimu Tanzania Bw.
Gratian Mukoba
amesema wabunge watakapokuwa wakijadili bajeti ya wizara ya elimu
wiki ijayo watambue kuwa mgoggoro huo bado upo.
“Serikali
itambue bado hatuja kubaliana juu ya madai yetu, hivyo mgogoro bado
hupo pia wabunge watambue hilo ili serikali ijadiliane juu ya maslahi
ya walimu” Alisema Mukoba
Aidha
CWT iliamua kukubaliana na serikali kufanya majadiliano kwa faida ya
walimu na ustawi wa elimu katika kikao cha baraza la majadiliano
ambacho kilifanyika Mjini Morogoro tarehe 09 mpaka 10/12013 na
tukakubaliana kufanya kikao kingine Februari 2013
“Katika
kikao hicho tulitaka ongezeko la mishahara,posho kuongezeka kwa
asilimia 30 na asilimia 50 kwa walimu wa sanaa na walimu wa sayansi
asilimia 50 tu, lakini serikli haikutimiza hayo” alisema
CWT
ilipeleka mchanganuo unaopelekea uhalali wa madai yake, serikali
ilitakiwa kushugulikia madai hayo haraka kabla ya kuitishwa kwa kikao
kingine cha majadiliano na baadae CWT ilitimiza jukumu lake kwa
kukubidhi serikali Justification yake tarehe 06/02/2013 lakini
serikali ilikaa kimya. Alisema Mukoba
“Tulikaa
tena tarehe 21/03/2013 hukohuko Morogoro lakini serikali haikuja na
yale tuliyo hitaji nabadala yake iliripoti kuwa mchakato wa
ufuatiliaji offer bado unaendelea jambo ambalo halikuturidhisha”
Alisema Mukoba
CWT
waliomba fursa ya kumwona waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi
kupitia, mwenyekiti, makamu mwenyekiti na katibu wa baraza ambapo
tarehe 24 mpaka 25/05/2013 majadilihao hayo yalifanyika jijini Dar es
salaam. Alisema Mukoba
katika
kikao hicho, walihitaji Ongezeko mishahara kwa asilimi 100, posho ya
kuundishia (Teachers allowance) 55% kwa walimu wa sayansi na 50% kwa
walimu wa sanaa, posho ya 30% kwa walimu wanaofanyakazi katika
mazingira magumu. Mambo ambayo walitaka wabunge watambue kuwa bado
hayajatatuliwa
Hivyo
CWT imeitaka serikali kuwa na nia njema na ikubali kurudisha mioyo ya
walimu iliyokufa kwa kukata tamaa ilikufufua utendaji wao na
kuboresha elimu ya Tanzania.
Bajeti
ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2013/2014 kwa wizara ya elimu
na mafunzo ya ufundi inatarajiwa kusomwa mapema wiki ijayo huko
Bungeni Dodoma
EmoticonEmoticon