Waziri wa Habari Mhe. Fenera Mkandara |
Wizara ya habari imeomba kiasi cha shilingi Billioni 20 na ushee
ili kuweza kutimiza mambo mbalimbali katika wizara hiyo, ambayo iko chini ya
Waziri Fenela Mkandara ambaye hii leo amesifiwa kwa staili ya ya nywele
Katika hotuba hiyo waziri hakuweza kuzungumzia hali ya
usalama ya wana habari wana mateso na mauaji ambayo yamewakumba wanahabari kama
kifo cha David Mwangozi, Absolom Kibanda na hata kufungiwa kwa gazeti la
Mwanahalisi ambalo mpaka sasa aijulikani itafunguliwa lini
Hali hiyo ili mshangaza Mbunge wa viti maalum kupitia tiketi
ya chama cha Demokrasia na maendeleo Bi. Rebeka Mgodo ambaye alishangazwa na
hotuba ya Mhe. Fenera Mkandara kwa kuwasahau waandishi wa habari pamoja na
matatizo yao ambayo yako wazi kwa jamii yote
“Nashangaa kutoona hata sehemu moja katika hii hotuba ya waziri wa Habari juu ya mazingira magumu
yanayo wakabili waandishi wa habari, wala mauaji ya David Mwangosi aliye uwawa
na polisi huko Iringa”Alisema Rebeka Mgodo
Aidha, Bi Rebeka amewataka viongozi kutoa ushirikiano kwa
waandishi wa habari pindi wanapofuata au kuitaji ufafanuzi wowote kutoka kwao
ili kuweza kurahisisha ufanyaji kazi wa waandishi wa habari. Alisema Rebeka
Naye Mhe. John Mnyika pamoja na kupanga hoja yake kwa point nyingi
wakati akiomba hoja yake kuungwa mkono na Bunge ili waweze kujadili swala la
mauaji ya David Mwangosi
Mnyika aliitaka Bunge kutengua kanuni ya 64 – 1c inayo zungumzia
mbunge kuto zungumzia swala linalo subiri maamuzi ya chombo kungine hasa
mahakamani, ambapo John Mnyika litaka wabunge wamuunge mkono ili waweze
kuchangia na kutekeleza Ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadamu nchini
LHRC iliyoongelea juu ya mauaji ya David Mwangosi ambaye aliuwawa na askari
polisi September 2 mwaka jana huko mkoani Iringa
Kabla wabunge hawaja simama kuunga mkono hoja, Spika wa
Bunge Mhe. Anne Makinda aliingilia na kupinga hoja hiyo ambayo ilizimwa zyyy
kama Analogia ndani ya Bunge hilo
REJEA HAPO JANA
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda aliunga mkono hoja Mhe.Godfrey
Zambi ambaye alitaka Spika kukataa kusomwa kwa hotuba ya kambi rasmi ya
upinzani ambayo ili wasilishwa na Mbunge wa Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi
ambayo ni bajeti kivuli ya Wazara habari.
EmoticonEmoticon