REA: BILLIONI 800 KUFANIKISHA UMEME VIJIJI VYOTE NCHINI

Mkurugenzi Mkuu REA. Lutengano Mwakahesya 

 Wakala wa kusambaza umeme vijijini Ruraral Energy Authority (REA) watatumia kiasi cha shilingi Billioni 800 ilikufanikisha mradi kabambe wa kufikisha umeme vijiji vyote nchini, mradi ambao utakamilika kwa muda wa miaka 2

Akiongea na Blog hii, ofisini kwake mkurugenzi mkuu wa REA, bwana Lutengano Mwakahesya amesema kuwa, REA inategemea kwenda kwa kasi zaidi ilikukamilisha mradi huo ilikufikisha malengo waliyojiwekea


“Malengo tuliojiwekea nikufikisha asilimia 16% ifikapo mwaka 2015, na hii Bilioni 800 itafanikisha mradi huo kabambe tuliojiwekea” alisema Lutengano


Mkurugenzi Mkuu REA. Lutengano Mwakahesya  


Aidha alisema, Mpango huo utaanza pindi tu watakapo pata Wakandarasi ifikapo mwezi wa 5 ili kuendesha mpango huo natayari hatua za kuwapata zinafanyika.

Lutengano amesema, Kuna jumla ya Billioni 200 wanategemea kupata kutoka nchi ya Norway ilikukamilishia miradi 46 yakupeleka umeme vijijini.

“ Kama mlivyo sikia kwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kuna Bilioni 200, kutoka Norway ambazo zitasaidia kukamilisha mradi wa Billioni 800 tuliojiwekea” Alisema Lutengano




Pesa zinazotolewa na Norway watashirikiana nasi kuzisimamia ilikuhakikisha kuwa miradi inakamilika. Alisema

Katika miradi 46, kipaumbele itakuwa kwenye wilaya mpya 13 ambapo wataweka umeme kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya, Mashule na Hospitali, ikiwapamoja na maeneo ya Njiani ambako mradi huo utakuwa unapita. Alisema Lutengano



Watumiaji wa nishati ya umeme vijijini wameongezeka kutoka asilimia 2% hadi 7%, huku REA ikijipanga kufikia 16% ifikapo mwaka 2015.

Hatahivyo REA imepokea kiasi cha Bilioni 200 kutoka nchi ya Norway kufanikisha mradi wao ambao wataukamilisha kwa miaka miwili kuanzia hivi sasa,


EmoticonEmoticon