Great Rift Valley Mining
Summit (GRV) hii leo wamekutana nchini Tanzania kwa siku mbili
kuangalia njia za kuongeza mapato kupitia vivutio vya madini
Mkutano huo umehusisha
nchi zilizoko kwenye nchi za Bonde la ufa, miongoni mwa nchi hizo ni
Uganda, Malawi, Zambia, Ethiopia, Mozambique, na Kenya
Akiongea kwenye mkutano
huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele amesema
Lengo kubwa la mkutano huo ni kuinua mapato yanayopatikana kwenye
madini, pamoja na kuweka mazingira mazuri ya watanzania kuwekeza
katika madini” alisema Masele
“Lengo kubwa ni
kuainisha vivutio vya uwekezaji kwenye madini ilikuongeza mapato ya
serikali” Alesema Masele
Aidha Masele amesema,
tayari wameanzisha mfuko maalum wa kuudumia mazingira na watu wanao
zunguka maeneo ya migodi ambayo inasaidia katika ujenzi wa mashule,
barabara na Hospitali ikiwa pamoja na kutunza mazingira ya maeneo
husika. Alisema
Naye Mtendaji mkuu wa
mamlaka ya ukaguzi wa madini nchini (TMMA)
Bwana Paul Masanja amesema
jumla ya shilingi Billioni 480 zimekusanywa na mamlaka hiyo kwa muda
wa miaka 3 toka kwa makampuni makubwa ya madini nchini
“Jumla ya Billioni 480
zimekusanywa kwa miaka 3 toka makampuni makubwa nchini ambayo
yanafanya biashara ya madini, kiasi hiki ni faida kwa taifa” na
kuongeza kuwa kiasi hicho ni sawa na nusu ya faida ya asilimia
15.51% ya faida ambayo taifa inapata kulinganisha na wawekezaji.
Bwana Paul Masanja alisema
kuwa, Tangu mwaka 1998 mpaka 2012 serikali imepata faida ya jumla ya
shilingi Trillioni 12.6 ambayo nayo imekusanywa kwenye mapato ya
migodi yote hapa nchini
Aliongeza kuwa, Kwa muda
wa mwaka mmoja serikali inakusanya kiasi cha Billioni 1.4 kama
makusanyo yatokananayo na madini ya ujenzi tofauti na ilivyo kuwa
hapo awali, ambapo serikali ilikuwa inakusanya Millioni 3 tu kutoka
kwenye madini hayo
Kamishna wa madini nchini
bwana Ally Samaje amesema fursa za kumiliki hisa kwa watanzania
ninyingi kuliko wageni kwani mtanzania anapaswa kuwa na hisa ya kiasi
cha asilimia 25% zaidi ya wageni ili kuwawezesha kunufaika na madini
hayo
EmoticonEmoticon