AJALI YAUWA WANDISHI TANGA, YUMO NA AFISA UHAIMIAJI


Hussein Semdoe Enzi za Uhai wake


Ajali Mbaya imetokea leo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga na kusababisha vifo vya watu watatu ambao ni waandishi wa habari wawili kutoka makampuni ya Mwananchi Communication na Uhuru Radio pamoja na Ofisa Uhamiaji.

Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa nne asubuhi iliuhusisha msafara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Muhingo Rweyemamu msafara unaodaiwa kuwa ulikuwa na magari matatu tu lakini gari moja liliacha njia na kupinduka 

Waliofariki ni pamoja na Hussein Semdoe mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Hamis Bwanga wa Radio Uhuru na Abood pamoja na Mariam Hassan ambaye ni Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Handeni.



Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo pamoja na vifo vya marehemu hao. Akizungumza na tovuti ya habarimpya mchana huu, Mkuu wa Wilaya hiyo alisema ajali hiyo imetokea wakiwa kwenye msafara kuelekea Ndolwa kupanda miti.

Muhingo ameiambia tovuti yako ya www.habarimpya.com kuwa gari lililopata ajali ni la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni, STJ 4673 ambalo ndilo lililokuwa likitumiwa na Ofisa Uhamiaji, Hassan pamoja na wanahabari hao.

Amesema msiba huo  mkubwa kwa Wilaya ya Handeni kwani wamepoteza wachapakazi na watu muhimu katika mchakato wa maendeleo ya wilaya hiyo. Aliongeza kuwa Wilaya ya Handeni imepoteza wanahabari kwa asilimia 100, kwani waandishi hao ndiyo waliokuwa wanahabari pekee wilayani hapo

. “…Msiba huu ni mkubwa si kwa tasnia ya wanahabari pekee bali hata kwa juhudi za maendeleo ya Wilaya ya Handeni, tulikuwa tukizunguka nao katika shughuli mbalimbali hapa Wilayani hivyo ni pigo kubwa,” alisema muhingo.


EmoticonEmoticon