KUTOKA BUNGENI
Wabunge hii leo wame yapokea mabadiliko kadhaa ya taratibu za uendeshaji bunge yaliyotolewa na naibu spika Mhe. Job Ndungai ambapo uwasilishaji utazingatia muda wa dakika 10, huku nafasi za shukrani zikiwekwa kando.
sambamba na Naibu spika kuelezea faida ya mabadiliko hayo yaliyoafikiwa na wabunge, hapo awali wabunge walikuwa wakitumia muda mwingi kuwashukuru watu wengi kituambacho kilikuwa kikipoteza muda mwingi.
Utaratibu huo, utaanza kutumika muda wowote wakati ofisi ya waziri mkuu ikiwasilisha hotuba yake ambayo itajumuisha wizara zote zilizo chini ya wizara hiyo.
*****************
Serikali bado inasubiri majibu ya Tume iliyoundwa kushugulikia janga la taifa la 2012 kwa matokeo ya kidato cha nne iliyoundwa na waziri mkuu. Mhe. Mizengo Pinda
Naibu Waziri wa Elimu-Tamisemi mhe. Kassim Majaliwa amesema hayo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Lushoto mhe. Henry Shekifu aliye taka kufahamu ni mpango gani wa makusudi wa serikali juu ya kushuka kwa elimu nchini.
**************
Mhe. Chalz Chizeba amesema hii leo bunge kuwa kupanda kwa bei za usafiri nchini (NAULI) kunatokana na kupanda kwa bei ya mafuta, alipokuwa akijibu swali lililo ulizwa na mbunge wa viti maalum Mhe. Diana Chilolo wakati wa maswali na majibu
Aidha Chizeba amesema siyo rahisi kwa serikali kudhibiti bei ya nauli za usafiri wa anga kama ilivyo kwa usafiri wa nchi kazu na chini ya sumatra, pamoja na kuwepo kwa TCAA hapa nchini kutokana na taratibu za safari hizo.
Mapema leo Bungeni
Uncategories
MUDA WA SHUKRANI ZISIZO NA MSINGI ZAPIGWA STOP BUNGENI, SERIKALI BADO INASUBIRI TUME ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA JANGA LA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon