RAIS ALIA NA MGONGANO WA KIDINI NCHINI, AGUSIA NYARAKA NA MATAMKO YANAYOTOLEWA , ASHANGAA KILA DINI KUILAUMU SERIKALI INAPENDELEA UPANDE MWINGINE, ASIHI WATANZANIA KUDUMISHA AMANI,UPENDO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr Jakaya Kikwete amesema kuwa kitendo cha kila upande wa kidini kuilaumu serikali kuwa ina pendelea upande mwingine, sio kweli kwani serikali inajali dini zote. Rais amekuwa akihutubia taifa kila ifikapo mwisho wa mwezi katika hotuba ya mwezi huu mambo ya kidini yalichukua nafasi kubwa
Akiongea Ikulu
Jijini Dar es salaam, Rais amewataka watanzania kuishi kwa upendo,
umoja na mshikamano na kuachana na malumbano ya Kidini yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani ambayo ndio
tunu ya taifa letu
“Kumekuwa na lawama kutoka kwa
Waislamu kuwa serikali inapendelea Wakristo na nchi inaendeshwa kwa
mfumo wa kikiristo,huku Wakristo nao Wakiilaumu serikali kuwa
inawapendelea Waislamu na kutochukua hatua zozote zile pale makanisa
yanapo chomwa kituambacho serikali inaangalia kwa kila upande bila
kumpendelea mtu” AlihutubiaRais
Rais Kikwete amesema, Serikali iko
dhabiti katika kulinda usalama wa Raia wake, Viongozi wakidini
Mashehe pamoja na maaskofu, na malizake na kusisitiza kuwa sikweli
kuwa serikali aichukui hatua zozote pale kunapotokea machafuko au
uvunjifu wa amani unaohusiana na maswala ya kidini
“Kutokana na Kuchomwa kwa makanisa,
kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa viongozi mbalimbali wa kidini pamoja
na mambo yanayoendana na hayo, Haimanishi Serikali imeshindwa kulinda
watu wake au inamaanisha serikali aichukui hatua zozozote”
Alihutubia Rais
Rais Kikwete amesema, Serikali
imechukua hatua nakuwa tayari waliohusika wameshikiliwa, huku
akieleza kuwa bado haija bainika moja kwa kama kama kuna kikundi
kinacho husika na matukio yote, huku akisema kuwa bado uchunguzi wa
kipolisi unaendelea ilikupata jibu sahihi
Aidha, aliongeza juu ya Nyaraka na
Matamko mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa Kidini kuwa yanaweza
kupelekea hisia za machafuko na uvunjifu wa amani, na kuwaomba
viongozi wa dini zote kuombea taifa liwe na amani. Pia amegusia swala
la misikiti 3 jijini Dar es salaam kumuombea Itikafu ili afe ikiwemo
Mkuu wa Majeshi nchini pamoja na Mkuu wa Kanda maalum ya Kipolisi ya
Jijini Dar es salaam
RAIS JK AAGIZA WALIOHUSIKA NA UZEMBE
WAKUBOMOKA JENGO LA GOGORA 16 WACHUKULIWE HATUA HARAKA
Katika Hotuba hiyo Rais alizitaka
mamlaka husika kuwachukulia hatua za haraka wale wote waliohusika na
uzembe na kupelekea jengo la gorofa 16 kuporomoja na kusababisha vifo
vya watu 30 huku wengie 17 wakinusurika kifo,
Rais amesema kuwa kutokana na hali ya
eneo la tukio nidhahiri kuwa hali hiyo ingeweza kuzuilika huku
akizitaka mamlaka zinazo husika kuweka njia za kuzuia matukio kama
yaho yasiweze kutokea tena, na kuagiza hatua za kisheria zichukuliwe
didhi yawale wote waliohusika na uzembe huo
Hatahivyo Rais alitoa shukrani kwa
Jeshi la Polisi, vikundi mbalimbali pamoja na watu waliojitolea
kuhakikisha kuwa wana wafukua waliofukiwa kwenye kifusi cha jengo
hilo ikiwa ni pamoja na kuwapa pole wawewote walifiwa na ndugu na
jamaa zao
RAIS ATOA WITO KWA WAANDISHI WA HABARI
Akiongea katika hotuba yake, Rais
amewataka waandishi wa habari kutoandika habari ambayo inalenga
kuchochea vurugu za kidini kwani kutofanya hivyo kunaweza kupelekea
kupotea kwa amani ya nchini yetu na kutolea nchi jirani ambazo tayari
zimewaikukumbwa na machafuko
Aidha amewataka wamiliki wa vyombo vya
habari kutoruhusu mtu kutoa habari inayolenga kukyza tofauti za
kidini nakuomba ushirikiano nao katika kukemea na kuelimisha jamii
juu ya tofauti zao ili pasiwepo na tofauti hizo
EmoticonEmoticon