Prof. Ibrahim Lipumba amewataka
watanzania kutunza muungano na kuachana na mawazo ya kuuvunja
muungano licha ya matatizo yaliyopo.
Prof. Lipumba ame yasema hayo hii leo
jijini Dar es salaam, alipokuwa akiongea na vyomba vya habari,
katika
makao makuu ya chama hicho.ambapo amesema tuangalie zaidi juu ya
kushugulikia matatizo ilikudumisha muungano kwa maendeleo ya wote
“Watanzania wengi wanaangalia juu ya
changa moto zilizopo na badala ya kushugulikia matatizo yaliyopo
ilikuweza kusonga mbele kama taifa” Alisema Lipumba
Nikweli kuna matatizo ya muungano, hata
mimi ninayajua lakini hayo hayawezi kutufanya kuuvunja muungano, bali
tujikite kwenye njia ambazo zitatuwezesha kuujenga muungano huo.
Alisema
Kesho maadhimisho ya muungano
yatafanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi wa juu watahudhuria
sherehe hizo, ikiwa ni miaka 49 ya muungano
Aidha kutokana na vurugu zilizo vuka
huko Liwale mkoani Lindi, Prof. Lipumba amewataka wakazi wa maeneo
hayo kuachana na maandamano na kuishauri serikali kukubali kukaa
chini na wakazi hao kujadili juu ya swala hilo
Hapo jana vurugu vilizuka miongoni mwa
wakulima na vyama vya sushirika vya Korosho mkoani Lindi baada ya
kutoafikiana juu ya bei halali ya kununulia bidhaa hizo
Prof. Lipumba ameitaka serikali
kuwalipa fedha wakulima hao kama walivyo ahidiana kwenye kikao cha
mauzo kilicho fanyika mwaka 2012
“Wananchi wali kabidhiwa Tsh. 200/=
kwa kilo badala ya shilingi 600/= kama ilivyo ahidiwa na kukubaliwa
kwenye mkataba wa mauzo, serikali nilazima iwalipe wakulima kulingana
na walivyokubaliana” Alisema
Serikali ifanye utafiti juu ya swala
hili, na kuunda chama cha wakulima wenyewe kuuza korosho hizo hili
haya yasijirudie. Alisema
Prof. Lipumba pia aliongelea swala la
matusi bungeni na kuwataka wabunge kuwa tambua watanzania walio
wachagua kuwa hawa vutiwi na hali hiyo hivyo kuacha mara moja.
EmoticonEmoticon