Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali
hii leo, imeunda tume ya watu watatu ili kuchunguza sababu za
kutokuwepo kwa mtambo wa kupimia mafuta bandarini yani Flow Metre,
ambayo haipo bandarini hapo tangu Februari mwaka 2011 hali inayo
ipotezea serikali mapato
Mhe. Zitto Kabwe ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo amesema Kamati yake imefikia uamuzi huo baada ya kuona kuna mvutano juu ya kutokuwepo kwa Flow Metre bandarini
“Mvutano uliopo kati ya TPA, TRA na
Wakala wa vipimo Tanzania, Kamati itaunda tume yawatu watatu nikiwemo
mimi, ilikufanya uchunguzi juu ya hasara inayotokana na kutokuwepo
kwa mtambo huu ambao unaijulisha Serikali nikiasi gani cha mafuta
kimeingia nchini ” Alisema Zitto
Katika kikao hicho mvutano mkali
ulikuwepo katiya TPA na Wakala wa Vipimo Tanzania ambapo Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania Bi. Magdalena Chuwa na Alekzander
Ndibalema kutoka TPA walikuwa wakivutana juu ya kutokuwepo kwa mzani
huo wakupima mafuta Bandarini
Picha zote na thecampasvision |
“ Bi Magdalena Chuwa alidai mtambo
huo uliharibika nakuwa wamepata malalamiko toka kwa wadau mbalimbali,
naye Alekzander Ndibalema akidai kuwa mtambo huo aujaharibika” kila
mtu alimtupia lawama mamlaka nyingine juu ya kuharibika kwa mtambo
huo
Mtambo wa kupimia mafuta bandarini Flow
Matre ulinunuliwa tangu mwaka 2004 hadi kuharibika mwaka 2011,
kituambacho kimesababisha mafuta kuingia bandarini Tanzania bila
kuwepo na uhakika wa kiasi gani cha mafuta kimeingia kutokana na
kutokuwepo kwa mtambo huo wa kupima mafuta.
EmoticonEmoticon