JUMLA YA WATOTO ELFU 58OO WAKO MTAANI DAR


Maandimisho ya Siku ya Mtoto wa Mtaani inatarajia kufanyika hapo kesho katika viwanja vya DON BOSCO jijini Dar es salaam, kauli mbiu ukiwa ni MTAANI NDIO NYUMBANI KWETU

Siku ya watoto wanao ishi na kufanyakazi mtaani kote Duniani, ilianzishwa ilikutoa fursa kwa watoto wamtaani kuzungumzia masuala yanayo husu haki za zao pamoja na kutafuta suluhu yakuondokana na tatizo hilo




Akiongea na Blog hii, Project Coordinator kutoka kituo cha watoto yatima cha Dogodogo Centre (DOGODOGO CENTRE STREET CHILDREN TRUST) Sabas B Masawe, aliomba jamii kwa ujumla kujitokeza siku hiyo ilikufahamu ni matatizo gani yanawapata watoto wa mtaani hapa nchini




“Wengi wetu tunadhani watoto wa mtaani ni yatima tu aliye kosa huduma za kijamii, au niwatukutu, waliotoroka kwao kwa makusudi, ila zipo sabau nyingi ambayo jamii inapaswa kutambua, hivyo tunawaalika waje kesho” Alisema

Masawe alisema, wengi tunawachukulia watoto wa mtaani kama wakosaji nilazima jamii na vyombo vya dola watambue kuwa watoto hawa wanaitaji msaada kwa wakati unao endana na kila mtoto, alisema




Jumla ya vituo 5 vya watoto ya tima hapa jijini ambao ni Dogodogo Centre, Kiwohede, Jukwaa la haki la watoto, GNRC Afrika pamoja na Vijana Vipaji Foundation wame andaa maadhimisho hayo.

Hatahivyo jumla ya watoto Elfu 5,800 wako katika mitaa ya jiji la Dar es salaam wakiomba omba hapa na pale bila msaada kutoka kwenye taasisi husika hapa nchini


EmoticonEmoticon