Jaji mkuu Frederick Werema amewataka wanasheria kuondoa malalamiko ya watanzania juu ya mikataba mibovu kwa kupitia upya mikataba ambayo imeshapitishwa ili kuokoa rasilimali za Taifa
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipokuwa akifungua mafunzo ya sheria ya makubaliano ya kibiashara kwa wanasheria 40 wa Serikali.
Jaji Werema amesema, wanasheria nilazima waamuke na kuomba kuipitia upya mikata upya na waangalie niwapi walikosea ilikuifanya kazi yao kuwa ya weledi na tija kwa taifa.
“Kama sisi tusipo sema wanachi watasema, waandishi kupitia makala na magazeti watasema, nilazima tuseme penye mapungufu bila kumuogopa mtu” alisisitiza Jaji Werema
Jaji Werema alisisitiza kuwa mengi ya tokea yakuibiwa rasilimali zetu yanasababishwa na makosa ya sheria, hivyo tuamke kwani maendeleo ya watanzania yako mikononi mwetu. Alisema kwa msisitizo
“Tuwalinde watanzania na mikataba mibovu (FEKI)tunayo simamia kama wanasheria .. makosa kama ya IPTL, DOWANSA nanyingine yasiwepo kwani makosa mengi yakuibiwa yanasababishwa na makosa ya kisheria” alisema
Pia amewataka wanasheria kujifunza lunga mbalimbali ilikuweza kukabiliana na wawekezaji mbalimbali kwani hiyo itawasaidia kuwa na uwezo mkubwa wakuchambua sheria mbalimbali huku akisisitiza juu ya sheria ya – Tanzania Investment Act[CAP 38 R.E 2012]
Aidha amesema, watanzania wengi hawajui kuwa watungasheria ni wabunge ambao huruhusu mikataba inayo walinda wawekezaji hivyo kuwataka wanasheria kuiwasimamia.
Mafunzo
kwa wanasheria hao 40 itafanyika kwa wiki moja lengo ikiwa ni
kuwafundisha juu ya kuingia makubaliano ya mikataba ya kibiashara.
Mpango uliofadhiliwa na UNDP. Mafunzo hayo yatafanyika shule ya
sheria (Law School of Tanzania)
kwamuda
mrefu sasa nchi imekuwa ikipoteza rasilimali zake kutokana na
mikataba mibovu inayopitishwa na viongozi pamoja na wanasheria.
EmoticonEmoticon