Mwenyekiti wa mtaa wa |
Kata 3 katika
Manispaa ya Kinondoni zimeshindwa kupata wa wakilishi wao katika
Mabaraza ya katiba ya Wilaya kwa kile kilicho daiwa kuwa ni itkadi za
kisiasa
Akiongea na Blog
hii kwanjia ya simu, Msemaji wa manispaa ya Kionondoni Bwana.
Sebastian Mhowera amesema kata hizo zimeahirisha wenyewe uchaguzi huo
hivyo hazita kuwa na wawakilishi wake katika Baraza la wilaya kwani
siku iliyo teuliwa kwa shuguli iyo tayari imemalizika.
Zoezi kwa
manispaa ya Kinondoni imekamilika isipokuwa kata 3 zimeshindwa
kufanya uchaguzi, wanaichukulia zoezi hili kama nila kisiasa jambo
ambalo haliusiani na zoezi la leo, Alisema Mhowera
Mhowera alitaja
kata hizo kuwa ni Kata ya Alimauwa A - Mtaa wa Kijitonyama, Kata ya
Kisiwani – Mtaa wa Makumbusho pamoja na Kata ya Mburahati – Mtaa
wa barafu., ambazo zimeshindwa kufanya uchaguzi huo
Aidha Blog hii
ilifanya mahojianao na Mwenyekiti wa mtaa wa Mzimuni kata ya Makumbusho Bwana Abdi Alyy, ambaye amesema katika kata yake waliomba
wananchi 72 huku wakiudhuria watu 80 katika uchaguzi huo
“Watu wengi
waliomba lakini tume wachagua 8 tu kulingana na utaratibu ulivyo
wekwa, zoezi lilikuwa salama na haki nawanachi wamechagua wenyewe
walio waitaji na mimi nitawakilisha majina yao” alisema Bwana Ally
Ally,
aliwashukuru wakazi wakata yake kwa kujitokeza kwa wingi katika
uchaguzi huo hali iliyopelekea kusiwepo na malalamiko yoyote wala
changa moto kwenye uchaguzi huo
Mchakato wa
kuandaa katiba mpya unaendelea, na hivi sasa imemalizika hatua ya
kutafuta wajumbe wa mabaraza ya katika ya kila mtaa ambao utaunda
mabaraza ya katiba ya wilaya, ambapo watawakilisha wananchi wengine
katika ukusanywaji wa maoni ya katika mpya ambapo Wajumbe hao ni 8 kutoka kila mtaa kama ilivyo tolewa na Jukwaa la katiba nchini
EmoticonEmoticon