NEW BAGAMOYO ROAD PROJECT - NDOTO KUMALIZIKA AUGUST 2013



Bango likionyesha mradi huo unakamilishwa chini ya watu gani.



Barabara ya New Bagamoyo road ambayo inajengwa na serikali kwa kusaidiana na watu wa Japan, hivi sasa ujenzi wake unasuasua licha kuwa bado miezi 4 tu barabara hiyo kukabithiwa kwa serikali

Ujenzi wa barabara hiyo unaofanywa na kampuni ya KONOIKE ina zua adha kwa watumiaji wa barabara hiyo hivi sasa kutokana na kuwekwa kwa road block kibao na ujenzi unaoendelea ambao hauna matumaini ya kumalizika kwa muda ambao uliwekwa na serikali 

Barabar hii ina madaraja 3, moja nila Lugalo jeshini karibu na mwenge maarufu kama Soza, la pili ni la Mbezi Beach maarufu kama Bondeni huku la 3 ni la tegeta kwa ndevu, katika haya madaraja ni upande mmoja tu ndio umekamilika huku upende wa pili ukisuburi neema za wakandarasi hao


Barabara hii inatokea mwenge mpaka tegeta kibaoni, hivi sasa foleni ndio kilio chetu tukisubiri rehema za KONOIKE, TANROADS,JAPAN na SERIKALI kwa ujumla kuokoa hii adha maana sasa neema imegeuka shubiri kwa wakazzi wa jiji wanao tumia barabara hii




EmoticonEmoticon