UHOLANZI YATOA BILLIONI 275 UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE, MWAKYEMBE NAYE AWAPIGA MKWARA WAKANDARASI


Picha ikionyesha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere

Waziri wa uchukuzi Mhe. Harison Mwakyembe ametoa onyo kwa makandarasi wa babaishaji, wasidhani kuwa Tanzania ni kichaka cha kuja kuzolea fedha na kuondoka

Waziri Mwakyembe ame yasema hayo hii leo jijini Dar es salaam wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa jengo jipya la abiria (TB III) katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere

“natoa onyo kwa makandarasi wa bababishaji. Wasidhani Tanzania ni kichaka cha kuja kuzolea fedha na kuondoka, katika ujenzi huu makandarasi watakao simamia nilazima wahakikishe kazi ina malizika kwa muda wa makubalianao yetu kwani kinyume na hapo sheria ya mkataba utafuatwa” Alisema Waziri

Utiaji saini ukiendelea kati ya Tanzania na Uholanzi

Ujenzi wa Jengo hilo unafanywa kwa msaada wa nchi ya Uholanzi, ambapo nchi hiyo imetoa kiasi cha Billioni 275 kukamilisha jengo hilo ambalo litajengwa kwa muda wa miaka 3 kuanzia hivi sasa, Aidha ujenzi wa Jengo hilo utawavutia wawekezaji na mashirika makubwa ya ndege kuleta huduma yako katika Viwanja vya Tanzania

“Mara baada ya mradi huu kukamilika, tunatarajia makampuni makubwa kuleta ndege zao hapa nchini, kuongeza pato la taifa na kuifanya Tanzania kuwavutia watalii wengi zaidi kuliko ilivyo sasa” Alisema Mwakyembe

Naye Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) amesema, Jengo jipya linalo tarajiwa kujengwa litajengwa kwa awamu mbili, ambapo utausisha maegesho ya ndege (APRON) barabara za viungio (TAXIWAYS) maegesho ya magari na barabara ya kuingia kiwanjani

Balozi wa Uholanzi akiongea kwenye utiaji saini huo

Bwana, Suleiman amesema kuwa, Ujenzi wa awamu ya kwanza utakuwa na ukubwa wa mita za mraba 35,00 Elfu wenye uwezo wa kuhudumia abiria Millioni tatu kwa mwaka, huku ujenzi wa awamu ya pili utakuwa na ukubwa wa mita za mraba 25,00 Elfu ukuwa na uwezo wa kuhudumia abiria Millioni Mbili na nusu kwa mwaka.

“Jengo jipya litakuwa na uwezo wa kubeba abiria Millionmi 6 kwa mwaka , pindi ujenzi wa wamu zote mbili kukamilika, lakini mradi uliosainiwa leo utagarimu kiasi cha EURO 133,228,145.45 sawa na pesa za kitanzania Billioni 275” alisema Suleiman

Kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TAA bwana Suleiman Suleiman akitia saini hapo jana, Nyuma kabisa yupo Waziri wa Uchukuzi Mhe. Mwakyembe

Hivi sasa kiwanja cha kimataifa cha Julius Nyerere kina uwezo wa kuhudumia abiria Milioni 1.2 hadi 4.7 kwa mwaka

Aidha baada ya mradi huo kukamilika kutaiwezesha TAA, kuwatenganisha abiria wanaosafiri ndani ya nchi (Domestic Passengers) ambapo abiria wanaosafiri nje ya nchi (International passengers) watatumia jengo jipya (TB III) na abiria wandani watatumia (TB II)


EmoticonEmoticon