> SIFURI ZA MTISHA ZITTO
> ASISITIZA WIZARA YA ELIMU
IAMISHIWE OFISI YA RAISI
> AMTAKA WAZIRI AWAJIBISHWE
> AHOJI JUU YA ELIMU YA VYUO VYA
UFUNDI, AKITABIRI TAIFA LA MAMBUMBUMBU
> ASISITIZA BILA ELIMU NIBURE
Taarifa ambayo Mbunge wa Kigoma
Kaskazini Zitto Kabwe ameiandika kwenye ukurasa wake wamitandao ya
kijamii,kuusiana na matokeo ya kidato cha nne 2012, ambapo mbunge
huyo ameitaka wizara ya Elimu kuwajibishwa na kuiamisha kwenda ofisi
ya raisi
Tarifa ya Zitto inasema, Matokeo ya
Kidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu kupata sifuri)
na takribani asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne na daraja la
sifuri kwa mwaka wa tatu
Zitto amesema kuwa,Waziri
lazima awajibike na Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna, Najua kuwa
haina uhusiano wa moja kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa
sana nchini. Lakini ni lazima kitu fulani kitokee ili kufanya
mabadiliko. amesema zitto
Aidha amesema, Tumwambie Rais aichukue Wizara ya Elimu, yaani Waziri wa Elimu awe yeye (kuwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Elimu). Tumwambie matokeo yakibaki hivi mwakani na yeye atatoka. kwani kwa kutofanya hivyo mwakani pia haya yatajirudia.

Mhe. Zitto ameendelea kusema, Mwaka jana tulisema mpango wa kujenga vyuo
vya ufundi kila Halmashauri ya Wilaya uanze mara moja. Katika Bajeti
Kivuli mwaka 2011 tulipiga hesabu kwamba tunahitaji tshs 720 bilioni
katika kipindi cha miaka 5 ijayo kujenga vyuo vya ufundi vya VETA
kila Wilaya.
Aliongeza kuwa, Tukawaambia badala ya kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya
jamii kulipana posho ni vema tukope kuwekeza kwenye elimu maana Elimu
ni Hifadhi ya Jamii. Elimu yetu ya sasa inazalisha matabaka kwenye
jamii na ni hatari sana kwa uhai wa Taifa.
Aidha, Tunaweza kujidai kujenga madaraja na miji mipya. Tunaweza kujidai kujenga mabomba ya gesi na kusambaza umeme kila kijiji mpaka kwenye vyoo. Kama hakuna Elimu haya yote ni bure kabisa. Hata kukosa uvumilivu wa kiimani sasa hali itakuwa mbaya zaidi unapokuwa na Taifa la mambumbumbu. Waziri Shukuru Kawambwa na wenzake watoke. Watoke SASAalimalizia Zitto

UBORA
NA UFAULU KWA DARAJA KIDATO CHA NNE 2012
DARAJA
(division) |
IDADI YA WAVULANA | IDADI YA WASICHANA | JUMLA |
I | 1073 | 568 | 1641 |
II | 4456 | 1997 | 6453 |
III | 10813 | 4613 | 15426 |
IV | 64344 | 38983 | 103327 |
0 | 120664 | 120239 | 24090 |
Idadi ya matokeo kama ilivyo kwenye
jedwari nikwamba wanafunzi waliopata Division I ni Elfu 1641 katika
taifa zima, waliopata Division II ni Elfu 6453, Division III ni
Elfu15,426, Division IV ni Laki103,327 huku Division 0 ni Laki
240,903 matokeo ya kidato cha nne 2012
EmoticonEmoticon