Juliana Shonza wakati akikaribishwa CCM-Dodoma |
Juliana Shonza aibukia CCM, Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha (CHADEMA) amerudisha kadi ya Chadema nakuamia CCM akiwa pamoja na Mtela Allam Mwampamba aliyegombea jimbo la Mbozi kwatiketi ya Chadema.
Wamerudisha kadi hiyo hii leo Mkoani Dodoma kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya ccm inayoendelea mkoani hapo. Juliana na mwampamba
wamepewa kadi ya kuamia CCM na mwenyekiti wa CCM taifa Mhe. Dr.
Jakaya Kikwete
Juliana Shonza |
Mapokezi yao ndani ya
chama hicho yamekuwa yaaina yake, huku wakipewa nafasi ya kutoa
ushuhuda juuya kilichotokea ndani ya Chadema mpaka kufikia kufukuzwa
ndani ya chama hicho.
Hapo awali madai ya Chadema juu ya Juliana Shonza na kufikia hatua ya kuvuliwa uanachama na kuondolewa katika uongozi wa BAVICHA, uliofanywa na mwenye kiti wa Bavicha John Heche kwa madai ya kueneza siasa za maslahi binafsi na kile kilichodaiwa kuni kukiujumu chama hicho, na shutuma nyingine niya kusema uongo juu ya chama hicho
Juliana alikana taarifa hizo na kutangaza kuwa yeye ni mwanachama halali wa Chadema kwani hakupewa barua ya kumwondoa
EmoticonEmoticon