Leo usiku Wakazi wa mkoa wa Mwanza watahamia mfumo mpya wa kurushia matangazo wa dijiti, Kama ilivyo pangwa na TCRA
Akiongea
na Blog hii akiwa Jijini Mwanza, Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania Bw. Innocent Mungi amesema kwamba, wakazi wa Jiji la Mwanza
wamejiandaa na wako tayari kwenda kwenye mfumo mpya wa dijiti.
Bwana
Inocent amesema, Jiji la Mwanza na vitongoji vyake leo usiku saa 5
Dakika 59 na Sekunde 59 wanahama rasmi kwenda mfumo mpya wa dijiti,
huku akieleza kuwa wakazi waeneo hilo tayari walijiandaa mapema
Mwanza
ni mkoa wa Nne kuhamia katika mfumo mpya wa kurushia matangazo wa
dijiti baada ya Dsm, Tanga na Dodoma.
Kwa
mujibu wa ratiba ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliyotolewa
Disemba mwaka jana, mikoa ambayo itafuata katika awamu ya kwanza ya
uzimaji mitambo ya Analojia ni Kilimanjaro na Arusha mwezi wa 3
pamoja na Mbeya mwezi wa 4.
EmoticonEmoticon