Akisomewa mashitaka hii leo mahakani. Afrika Kusini |
Mwanariadha
mlemavu wa Afrika kusini Oscar Pistorius leo amemwaga chozi
wakati akisomewa mashtaka ya mauaji ya mpenzi wake katika mahakama ya
jijini Pretoria. Tukio alilofanya siku ya valentines day
Star
huyo wa mashindano ya Olympic ya walemavu mwenye umri wa miaka 26
alishika kichwa kwa masikitiko mara baada ya shitaka lake la kwanza
kutajwa na Hakimu wa mahakama hiyo
Akiwa uwanjani akijiandaa kukimbia (Marathon 2012) |
Hakutakiwa
kujibu chochote katika kesi hiyo ingawa ndugu, jamaa na uongozi wake
unapinga kwa nguvu zote tuhuma zote zinazoelekezwa kwake kwamba
alimuua kwa makusudi mpenzi wake Reeva Steenkamp, mwenye umri
wa miaka 29, alfajiri ya kuamkia siku ya Valentine
Waendesha
mashtaka wa kesi hiyo wameieleza mahakama kuwa yalikuwa ni mauaji ya
kukusudia na kupanga yanayostahili adhabu ya kifungo cha maisha
Aliposikia
hivyo, Oscar alishtuka kwa hisia kali sana za huzuni na uchungu
lakini hatahivyo baba yake mzazi pamoja na ndugu zake waliokuwepo
mahakamani hapo walimfariji na kumtia moyo
Oscar Pretorius akiwa na mpenzi wake huyo siku zanyuma |
Minong'ono
ilisikika mahakamani hapo baada ya bastola anayotuhumiwa kuitumia
katika mauaji hayo kuletwa mahakani hapo ikiwa ndani ya mfuko wa
Plastik ikiwa imebebwa na polisi
Vyombo
mbalimbali vya habari nchini Afrika K usini zimesema kuwa asubuhi ya
siku yatukio hilo, walimkuta Oscar akiwa amekaa pembeni ya mwili wa
Steenkkamp akiwa amekwisha kufa
EmoticonEmoticon