Kushoto,Waziri wa Elimu Mhe.Shukuru Kawambwa, Kulia Naibu wake Mhe. Philip Mulugo |
Kufuatia
matokeo mabaya ya mitihani kidato cha nne 2012, Mwenyekiti wa chama
cha NCCR Mageuzi na Mbunge wa kuteuliwa Mhe. James Mbatia
amesikitishwa na kiwango hicho na kusema kuwa hali hiyo nikukosa
usukani kwa elimu ya Tanzania.
Mbeshimiwa
Mbatia amesema hayo hii leo ofisini kwake jiji Dar es salaam,
akiongea na waandishi wa habari, ambapo alisisitiza elimu kuporomoka.
“Elimu
ya Tanzania inaporomoka kwa kukosa usukani na mwelekeo, kama maswala
haya hayatachukuliwa maanani swala la elimu litaendelea kuwa
kikwazo” Amesema Mbatia.
Akiongelea
swala la wastani waufaulu ambapo asilimia 60 wamepata ziro (Divisio 0
), asilimia 20 wamepata daraja la nne (Division IV), asilimia
iliyobaki haiwezi kukuza elimya ya Tanzania na kwamba hali hiyo ni
msiba kwa Taifa.
Mhe.
Mbatia amesema, sababu inayosababisha hali hiyo ni mfumo mbovu
usioeleweka wa Elimu pamoja na mitaala ya Elimu nchini ambayo
inawaongoza wanafunzi juu ya Elimu yao, alisema.
“Hakuna
mitaala inayoeleweka ya elimu nchini, pamoja na iliyopo hivi sasa
hii ndi inachangia elimu kuyumba, huku akiongea kwa masikitiko
makubwa” alisema Mbatia.
James Mbatia kulia |
“ Mitaala
hii sio halisi huku akikionyesha kwa wanahabari, aina no. ya ISB,
aina Nembo ya Taifa ya adam na hawa pamoja na saini hata ya mmiliki
wake” alisema Mbatia
Matokeo
ya kidato cha nne yalitangazwa jana na waziri wa elimu, huku
wanafunzi Elfu 1641 tu ndio waliopata Division I, Elfu 6453 ndio
wenye division II, Elfu 15,426 Division III, huku laki 103,327
wakipata Division IV na Laki 240,903 wakipata Division 0.
EmoticonEmoticon