PAPA MPYA KUJULIKANA KABLA YA PASAKA

  • KUJIUZULU KWA PAPA BENEDICT XVI
  • PAPA MPYA KUTEULIWA KABLA YA PASAKA
  • MAMBO MUHIMU USIYO YAJUA JUU YA PAPA



Makao makuu ya Kanisa katoliki huko Vatcan imesema yanatarajia kumpata papa mpya kabla ya mwisho wa mwezi watatu na kabla ya sherehe za pasaka.

Hii nibaada ya Kiongozi mkuu wa dini ya katholiki duniani Pope Benedict XVI, kutangaza niaya yakutaka kujiuzulu hapojana, kutokana na umri wake, Akitangaza uamuzi huo ambao amesema ifikapo terehe 28 mwezi huu ataachia ngazi rasmi hivyo kutoa nafasi kwa kiongozi mwingin.

Uwamuzi na hatua ya Papa Benedict XVI wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu ni baada ya kudumu kwa takriban miaka minane akiongoza Kanisa Katoliki nahivi sasa anaumri wa miaka 85 nahivyo hawezi kuongoza tena.


Papa Benedict, nimzaliwa wa Bavaria huko Germany na amezaliwa mwaka 1927 tarehe 16 mwezi wa Nne (April 16 1927) jinalake halisi ni Joseph Alois Ratzinger. Yeye ndiye mridhi wa Pope John Poll II aliyefariki dunia mwaka 2005, ambapo April 19 alisimikwa nakuwa Papa ikiwa nisiku chache tu baada ya tarehe yake ya kuzaliwa.


Papa Benedict xvi nimjerumani wa nane kuwa papa, nimsomi sana na anajua zaidi kutumi kinanda (Piano). Miaka ya 1943 akiwa anaitwa Ratzinger alijiunga na kundi la Hitler (Hitler youth) na akawa kama mwanajeshi huku anaumri wa miaka 14 tu.

Baada ya vita yapili ya Dunia (WORLD WAR II) alisomea thiologia nakuwa muhubiri mwaka 1951, miaka ya 50s – 60s alikuwa akifundisha katika chuo cha Ujerumani ( German Universities) nakatika kipindi hiki aliandika vitabu vingi vya elimu ya Thiolojia

Miaka ya 1977 na 1978 alikuwa Cardinali na Askofu mkuu, nakipindi hicho Marehemu Paul ii alisimikwa na kuwa Papa, nayeye nduye alikuwa mshauri wake. 

Baada ya John Pole II kufariki na pope Benedict xvi kuingia madarakani akiwa na miaka 78, kwa bara la Afrika alitoa maoni ya kukosoa matumizi ya Condom kwa watu wa Afrika kama nguzo yakuzui Ugonjwa huo kwani aliamini kuwa kuruhusu matumizi ya Condom nikuongeza matatizo juu ya kusambaa kwa ugonjwa huo.

Papa Benedict VXI ndiye kiongozi aliye teswa zaidi na skendo za Ushoka kwabaadhi ya viongozi wake wakuu, lakini alifanikiwa kuzima mahasi yao kwakiasi kikubwa na kwaupande mwingine ameweza kuleta mausiano mazuri kati yao na Waislamu.


EmoticonEmoticon