Upimaji uzito katika mapambano mawili ya IBF yanayofanyika
katika majiji ya Johannesburg na Tunis umemalizika vizuri hapo jana
Mapambano haya yaliyopewa jina la “Barabara ya kutoka Cape Town mpaka Cairo
kwa IBF” kutokana na majiji haya
kukaa moja kusini na lingine kaskazini mwa Afrika, yanafanyika wakati IBF ikijipanga
vyema katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Kusini mwa Afrika, leo imeshuhudia mabaondia mawili
wanaopambania ubingwa wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25 wakipima
uzito mbele ya mashirika mbalimbali ya habari ya ndani na nje ya Afrika ya
Kusini.
Illunga Makabu
kutoka Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) alipima uzito kumkabili Gogota Gorgiladze
wa Georgia. Upimaji huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa ulio
katika hotel ya nyota tano ya Emperors Palace iliyoko katika jiji la
Johannesburg!
Rodney Berman mtu anayeheshimika kwa kuwa promota wa
kwanza kuandaa pambano la IBF la dunia katika bara la Afrika mwaka 1990, ndiye
anayepromoti pambano hilo
Tayari wadau na mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi
mbalimbali za Afrika zikiwamo Namibia, Zambia, Msumbiji, Zimbabwe na Tanzania
wameshawasili nchini Afrika ya Kusini tayari kuangalia mpambano huo. Wengine
walibaki Afrika ya Kusini wakati wa mashindano ya kombe la Afrika
yaliyomalizika wiki iliyoita.
Msimamazi mkuu wa mpambano huu ni Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi aliyesimama
pichani na mabondia Gogita Gorgiladze (kushoto) na Ilunga Makabu (kulia)
HABARI ZA KASKAZINI
MWA AFRIKA
Bondia ambaye ameshajizolea sifa kemkem Ayoub Nefzi wa Tunisia anayeishi
nchini Belgium atapigana na bondia Ishmael
Tetteh kutoka nchi ya Ghana kugombea ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi
na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Light Middle.
Mpambano huo uliopewa jina la “Uzuri wa Jasmine” kutokana na jina hilo kutumika katika mapinduzi
yaliyomwondoa Rais wa zamani wa Tunisia Ben Ali unafanyika wakati Ayoub Nefzi akijiandaa kugombea mkanda
wa juu wa IBF wa mabara mwezi wa tatu nchini Belgium.
Mabondia wote wawili wanatagemea kuonyesha moto mkali
katika mpambano ambao tayari mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi za Nigeria,
Ghana, Libya, Misri, Algeria tayari wameshawasili nchini Tunisia kuangalia
mpambano huo!
Tunisia inasifika kama nchi iliyowahi kutoa viongozi wengi
wa mchezo wa ngumi katika bara la Afrika.
Habari picha imetumwa na Onesmo Ngowi, Rais wa IBF/AFRICA
EmoticonEmoticon