VITAMBULISHO VYA KWANZA VYA TAIFA VYA TOLEWA LEO


RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho kikwe leo ameongoza uzindua rasmi zoezi la Vitambulisho vya taifa uliofanyika jijini Dar es salaam hii leo wakutoa vitambulisho kwa viongozi wakuu waandamazi na wale ambao wamestaafu

Akiongea katika uzindua huo Rais Kikwete amesema, Ndoto ya sikinyingi ya taifa hili imetia yakuwa na vitambulisho vya Taifa japokuwa imepitia katika vikwazo vingi sana kwani tangu kipindi cha Rasi wakwanza wa nchii hii Hayati Kambarage Nyerere niyayakutengeza vitambulisho hivyo ilikuwepo

“Mchakato huu umekuwepo kwa muda mrefu lakini leo nisiku muhimu na nzuri kwa taifa nchi yetu, ndoto yetu ya sikunyingi hatimaye imetimia” aliosema Rais Kikwete

Amesema, Tangu Uhuru wa Tanganyika, mapinduzi matukufu ya Zanzibar, tangu muungano hadi hivi sasa, nahata kwa viongozi waliopita waliendelea kutafuta mchakato huu wa vitambulisho vya taifa

“ Mchakato huu umepitia vikwazo vingi, Wakati wa Mhe. Mkapa Serikali ilifikishwa mahakamani kwaajili ya hili swala na kuitupilia mbali, lakini mpango ukaendelea mpaka hivi sasa zoezi limekamilia” Alisema Rais Jakaya

Faida za vitambulisho vya taifa nikujua kila raia na mahali walipo kituambacho kitarahisisha kujua taarifa za wananchi wako na kiasi gani unaweza kuwasaidia ilikuinua uchumi

Aidha miongoni mwa faida ni kutarahisisha upatikanaji wa mikopo, na kuinua uchumi wa nchi na kusisitiza kuwa itawezesha usalama wakutoa mikopo kwani vitambulisho vitakuwa na taarifa zote za muombaji kituambacho kitampa sifa mtoa mkopo huo

Naye Mkurugenzi mkuu wa NIDA, Bwana Dikson Maimu amesema kuwa wakati wa uandaaji wa Vitambulisho hivyo kamati ilimepitia changamoto kadhaa ikiwemo ya wananchi wengi kukosa viambatanisho muhimu vya kumtambulisha natarifa sahihi zinazomuhusu.



“Mfumo wa maombi ya vitambulisho mtu anatakiwa kuwa na viambatanisho muhimu zakumthibitisha umri wake, makazi yake na uraia wake, vituambavyo wengi hawana” Alisema Maimu

Aidha mtuatakaye kosa viambatanisho hivyo ofisi ya serikali zamtaa unaouwezo wa kubaini kama anayepewa kitambulisho hicho ni mtu sahihi, Alisema Muimu

Viambatanisho ambavyo vinaitajika nikama Vyeti vya Kielimu, Vyeti vya Kielimu vya sekondari pamoja na viapo mbalimbali

Muimu amesema, Kutokana na tume ya uchaguzi kuituma maombi ya vitambulisho hivyo kutumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, tutashirikiana nao katika kutambua ilikufanya zoezi hilo kuwa lamuda mfupi

“ Ilikutoa ushirikiano kwa tume ya uchaguzi, jumla ya Computer elfu 12 zinahitajika ilikuweza kupata alama za vidole” Alisema Muimu

Bwana. Muimu ametoa rai kwa wananchi na wageni pamoja na wakimbizi na wale waliotimiza mika 18 wajitokeze kwa wingi katika zoezi hilo pindi litakapo fanyika kitaifa





EmoticonEmoticon