MASHALI AMTAMBIA CHEKA, ASEMA UZITO SIO KIGEZO, KUKIPIGA MAY MOSI


Francis Cheka (kushoto) akiwa na Adam Tanaka (katikatia) na Thomas Mashali (kulia)
Thomas Machali amemtambia bondia mwenzake Francis Cheka kuwa asitegemee uraisi katuika mechi watakayo pambana ifikapo Mei Mosi mwaka huu, kwani hayuko tayari kupoteza ubingwa wake wa Middle Weight 

"Mimi ninauzito wa Middle nayeye Cheka anauzito wa Super Weight lakini namwambia siogopi na nitapambana naye, kuwa na uzito wajuu sio sababu ya kuogopa nitapambana naye mpaka nitetee ubingwa wangu" Alisema Thoma Mashali

Naye Francis Cheka amesema, hana mashaka na mpambano huo kwani anamfahamu vizuri Mashali na kwamba atatetea upingwa wake ili watanzania wajue kwanini alishinda na kuwa anastahili kutetea ubingwa huo.

Francis Cheka anakibarua kigumu zaidi katika pambano hili ambalo Kama Francis Cheka atashinda tena pambano hili, atapewa nafasi ya kupigana kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF I/C) .


Aidha, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF/Africa) limetoa kibali kwa bondia Francis Cheka ambaye ni bingwa wa Africa katika uzito wa Super Middle kutetea ubingwa wake dhidi ya bondia Thomas Mashali wa Tanzania, ambapo wamesign makubaliano ya mpambano huo na kupewa nafasi ya kutambiana kibondia 

Mabondia hao wawili leo tarehe 13 February walikutana katika hoteli ya Ndekha, iliyoko Magomeni Kondoa na kutia sahihi mkataba wa kupigana pambano hilo ambalo limepangwa kufanyika siku ya Mei Day katika ukumbi wa PTA jijini dar-Es-Salaam.

Thomas Mashali ambaye ndiye bingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle ana kiwango kizuri cha kushindana na Francis Cheka katika pambalo hilo.


Hii itakuwa mara ya pili kwa bondia Francis Cheka kutetea mkanda alioushinda tarehe 29 April 2012 dhidi ya bondia machachari Mada Maugo wa Tanzania. Cheka aliutetea vyema mkanda wa ubingwa wa IBF/Africa dhidi ya bondia Chiotcha Chimwemwe ambaye ni Afisa katika jeshi la Malawi siku ya Boxing Day (26 Decewmber 2012) katika jiji la Arusha.


 Pambano hili linaandaliwa na kampuni ya Mumask Investment and Gebby Pressure ya jijini Dar-Es-Salaam chini ya uratibu wa Adam Tanaka! 


EmoticonEmoticon