Taarifa
ambazo zimetufikia hivi punde kupitia WAPO Radio FM, zinaeleza kuwa
huko mkoani Geita, kuna vita kati ya Waislamu na Wakristo, kufuatia
hatua ya Wakristo kuchinja mifugo kwa nia ya kuuziana wenyewe kwa
wenyewe kwenye bucha walilotenga.
Jambo
hilo linaelezwa kuzua tafrani kwa jamii ya Waislamu, kwani waliamua
kuvamia eneo hilo na kuharibu bucha, pikipiki eneo hilo, na
kusababisha watu kuingilia, na vita kuibuka, silaha za jadi
zikitumika.
HAPO
AWALI
Wakristo
Mkoani Geita eneo la Katoro na Buselesele, waliamua kuachana na
kununua nyama katika bucha za kawaida kwa madaikwamba hiyo ni ibada
kwa waislamu, na hivyo wao hawako tayari kushiriki ibada hiyo, na
badala yake watafanya ya kwao. Ndipo walipokwenda Kituo cha Polisi na
kuomba kibali cha kuchinja, ambacho walipewa ilmradi wasiuze nyama
hiyo.
hatimaye
Wakrsito hao wakachinja na kuamua kupeleka kwenye bucha lao ambalo
wamelitenga kwa ajili ya waumini wao kununua. Waislamu kuona hivyo,
ndipo wakaenda kuripoti kituoi cha Polisi, na wakati Polisi
(wachache) wanaongea na viongozi wa Kikristo eneo hilo ili kutatua na
kurejesha amani, ndipo kundi la Waislamu likaja na kuanza kushambulia
kilichokkuwa eneo hilo, wakivunja bucha, na pikipiki ya mkristo
mmojawapo iliyokuwa eneo hilo.
Hatua
hiyo imeelezwa kuibua hasia na kupelekea baadhi ya wat waliokuwa eneo
hilo kuanza kujibu mashambulizi hayo, na mpaka hivi sasa inaripotiwa
kuwa nguvu zaidi ya Jehi la Polisi haijafika eneo hilo, huku waumini
wawili wa dini ya Kiislamu wakiwa katika hali mbaya kutokana na
kipigo.
Silaha
ni za jadi, na eneo hilo haliko salama kwa hivi sasa, kwani hata
amduka mengine yamefungwa kuhofia usalama wa mali na maisha.
Akihojiwa
na Beatrice Kamanga, katibu wa umoja wa makanisa ya Katoro na
Buselesele, Mchungaji Silvanus Dominick, ameeleza kuwa kama hali
haitatulizwa mara moja basi eneo hilo laweza kuleta madhara zaidi.
Endelea
kufuatilia, nasi tutakuhabarisha kile ambacho kinaendelea kadri
ambacyo taarifa zitatufikia. na pia unaweza kufuatilia kupitia WAPO
Radio FM kwa kuisikiliza kwenye blog hii na tovuti ya WAPO.
EmoticonEmoticon