WAFUASI wa vyama vya CCM na Chadema wamechapana makonde hadharani jana Mkoani Dodoma, chanzo cha vurugu hizo zilitokana na wafuasi wao kugombea mti wa kutundika bendera za vyama vyao.
Vurugu hizo zilitokea karibu na Bar ya Mwanga, baada ya kada wa CCM kung'oa mtu uliokuwa ukitumiwa na Chadema kuweka Bendera ya chama chao na kisha wana CCM kutundika bendera yao katika eneo hilo.
Hata hivo vurugu hizo zilitulizwa na Askari wa Jeshila Polisi kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU).
Baadhi ya wabunge wa CCM walioshiriki katika vurugu hizo na majimbo
yao kwenye mabano ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Nyambari Nyangwine
(Tarime), Seleman Jafo (Kisarawe), Said Mtanda (Mchinga) na Mary
Chatanda (Viti Maalumu).
Habari na Habarimpya.com
EmoticonEmoticon