Baada ya wadau wengi kulalamikia mpango wa Matangazo ya Bunge kutorushwa live kama ilivyo kaririwa na vyombo mbalimbali vya habari kwa wiki moja sasa, Mpango huo umepigwa chini tena nakuwa matangazo hayo yatarushwa live kama ilivyokuwa hapo hawali
Akitoa taarifa hiyo katibu mkuu wa Bunge Dr. Thomas
Kashililah amesema kuwa ofisi ya Bunge haitositisha matangazo ya Bunge ila
itafanya maboresho mawasiliano kwanjia ya kawaida kupitia Teknohama ambapo
watakuwa na Television na Radio ambazo zinarusha matangazo hayo moja kwa moja
Dr, Kashililah amesema, Bunge litazindua Radio yake hivi
karibuni ambapo itatmika nchini zima, pia kutakuwa na matangazo ya moja kwa
moja kupitia kwenye mtandao mpya ambao utarusha matangazo hayo masaa 24. Aidha vituo vya Television vitaruhusiwa kurusha matangazo
hayo moja kwa moja bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote ikiwa ni sambamba na
matngazo yatakayo tolewa na mitambo ya Bunge
Kama ilivyo hapo awali Bunge halitarusha matangazo ya aina
yoyote ile isipo kuwa nakala ya majadiliano ya Bunge kwa mtu yeyote atakaye au kituo
cha Television na Radio vitaruhusiwa kupitia katika mitambo yake lakini nayo
iwe nakala ya majadiliano ya Bunge
Waandishi wa habari hawatapata furasa ya kuingiza kamera
ndani ya ukumbi wa Bunge, bali watapata picha hizo kutoka katika mitambo ya
Bunge nakurusha moja kwa moja. Alisema Dr. Kashililah
Bunge litatoa utaratibu (Code of conduct for media
broadicasting) wa namana ya kunakili na
kurusha matanngazo ya Bunge bila kujali
yanarushwa kwa utaratibu upi. Hii itasaidia kuweka misingi bora ya mawasiliano
na hivyo kuwapafursa wananch kujua hali halisi ya matukio yote ndani ya Bunge
na kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan) alisema Dr. Kashililah
Dr. Kashililah pia amekanusha swala la Bunge kurorushwa live
kuwa alinukuliwa vibaya na kusisitiza kuwa ni maboresho tu ndio yatafuata
lakini matangazo y a Bunge yatarushwa live kama hapo awali. Na wanachi
watajulishwa kila hatua ya mabadiliko hayo
EmoticonEmoticon