>MITAALA NIHALISI, KAMATI YASEMA
> Mhe.MBATIA NAE ASHIKILIA MSIMAMO WAKE, KUWA SIO
HALISI
> Mhe. KWAWAMBA AZIDI KUPONDA HOJAZEKE, ASEMA
AZINA MAANA
Bunge leo limepokea taarifa ya Tume
iliyoundwa kuchunguza uhalisi wa mitaala iliyowasilishwa na serikali, Tume hiyo
imedhibitisha kuwa mitaala
hiyowasilishwa Bungeni ni halisi na haijachakachuliwa.
Akiongea Bungeni, Spika wa Bunge Mhe. Anna
Makinda amebainisha kwamba nakala tatu zilizowasilishwa ya mitaala wa Elimu wa
awali, msingi na sekondari zote niza mwaka 2005 na ndio halisi
Kufuatia taarifa hiyo Mhe. James Mbatia ambaye
aliibua sakata hilo baada ya kuwasilisha hoja binafsi juu ya udhaifu ulipo
katika sekta ya Elimu nchini, Leo amesema kuwa mitaala hiyo sio halisi huku
akitoa sababu za kudhibitisha kauli yake hiyo
“Mitaala
hii sio halisi kwani kwani imekosa sahihi husika na haina namba za utambulisho
wa kimataifa, aiwezi kuwa halisi”Alisema Mbatia
Mhe. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya ufundi amesema Bungeni hapo, akijibu baadhi ya hoja za Mbatia kuwa
sababu anazotoa hazina msingi huku akisisitiza kuwa Siyolazima machapisho ya
ndani kama mitaala yawena udhibitisho wa kimataifa
Sakata la mitaala liliibuka Bungeni baada ya Mhe. Mbatia kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka kujadiliwa kwa udhaifu uliopo kwenye sekta ya Elimu. Miongoni mwa mambo aliyokuwa akilalamikia ni swala la mitaala ya Elimu kwa Shule za awali, msingi na sekondari
Pia Waziri aliwai kuahidi Bungeni kuwa angewasilisha mitaala kwa Wabunge kituambacho waziri huyo wa Elimu hakikutekeleza na wabunge wengi wa upinzani kupaza sauti na kusema hakuna mitaala hiyo
WABUNGE WAMKERA SPIKA WA BUNGE
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda ameonyesha
kukerwa na kukasirishwa na kitendo cha wabunge, kuhudhuria kwa uchache katika
vikao vya Bunge kitendo kilicho sababisha kuahirishwa kwa kikao cha saba, Spika
amewaambia wabunge kuwa wanapokuwa Bungeni Dodoma hawajipumzisha bali wako
kutekeleza majukumu yao ya Kibunge
Taarifa ambazo Blog hii imepata kutoka huko
Bungeni nikuwa siku hiyo ya kikao cha 7 jumla ya Wabunge 22 tu ndio
walihudhuria vikao vya jioni vya Bunge
EmoticonEmoticon