MADUKA 10 YATEKETEA KWA MOTO, ZAIDI YA MILIONI 250 ZAHOFIWA KUTEKETEA



Moto uliozuka katika Stendi ya mabasi mwenge unahofiwa kuteketeza zaidi ya Milioni 250 katika maduka 10 yaliyounguzwa na moto huo, huku mengine mengi yakinusurika katika tukio hilo


Kutokana na halikutokuwa ya utulivu katika eneo hilo Blog hii aikuweza kupata majina halisi ya wafanyabiashara hao ambao walilemewa na kazi ya kutoa vituvyao nje ya maduka huku wengine wakisikitishwa na motohuo


Wafanyabiashara hao wameeleza chanzo cha moto huo kuwa ni mfumo wa umeme wanao tumia ambao umeunganisha karibu maduka yote katika soko hilo, kituambacho nivigumu kuokoa kitu kama moto ukizuka katika eneo hilo
 

Wafanya Biashara wa Mwenge wameishukuru jeshi la Polisi kuweka ulinzi mkali na kunusuru vitu vyao ili visiibiwe pindi moto ukiteketeza maduka leo asubuhi katika eneo hilo


Blog hii ilishuhudia baadhi ya bidhaa zikiwa zimemwaga chini nje ya maduka sokoni hapo huku magari ya abiria yakizuiliwa kuingia kwausalama zaidi. 


EmoticonEmoticon