Barabara
ya Old Bagamoyo imebadilishwa jina rasmi nakuitwa jina la Raisi wa
Kenya anaye karibia kumaliza muda wake, Mwai Kibaki katika Uzinduzi
uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Raisi huyo mapema
hii leo jijini Dar es salaam
Akiongea katika uzinduzi huo, Rais Mwai Kibaki amesema Tanzania iseme inataka nini kwa nchi hiyo, nakuongeza kuwa majina yanapokuwepo inamaana ya uhusiano mzuri kati ya nchi yetu na nchi hiyo ilikuweka kumbukumbu" Alisema Rais huyo
Barabara
hiyo yenye urefu wa kilometa 10.1., ikitokea makutano ya Barabara ya
Rashid Kawawa hadi njia panda ya Africana na kukutana na Bagamoro
Road imebadilishwa jina na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Jakaya Kikwete
Uzinduzi
huo umefanyika Mbeye ya Waziri wa Ujenzi Prof. John Pombe Magufuli,
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadic na Meya wamanispaa ya
Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda. Na Jina la barabara hiyo imetolewa kama Eshima kwa raisi huyo anaye karibia kumaliza mda wake
Raisi
Mwaikibaki amebakiza muda wa wiki mbili ilikuachia ngazi ya Uraisi wa
Kenya mara baada ya Uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufanyika March 4
mwaka huu.
Hatahivyo baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam, walikuwa na maoni tofauti juu ya uzinduzi huo huku wakihoji nikitugani hasa,
Raisi huyo wakenya ameifanyia Tanzania kiasi cha kumpa sifa ya jina la barabara nchini Mwetu
Iddi Abdala, amesema " Bado sijajua kwa nini Raisi nawatu wake wameamua kubadilijina, nikitugani hasa ameifanyia Tanzania kiasi cha kuweka kumbukumbu au kama kuna kitu kimefichwa basi tuambiwe" Alisema Iddi
" Barabara hii inahistoria ya watumwa ambao walikuwa wakipita kupelekwa Bagamoyo enzi hizo, kuiita Mwai Kibabi inafuta historia yake, kimsingi sijaona alichokifanya Rais huyo kwa Tanzania kiasi cha kupewa jina hilo" Alisema Idd
Naye Suza Lyimo. amesema Akuna shida jina lake kuwekwa ndani ya nchi yetu akielezea kwamba sisi ni Afrika Mashariki tukiwa na umoja siombaya japo naye akujua nikwanini imeamriwa hivyo.
Watu wengi amboa Blog hii imefanyanao mahojiano walipinga sana uamuzi huo huku wakijiuliza nikitugani alichokifanya Rais huyo nchini mwetu.
EmoticonEmoticon