Kutokana
na serikali kuunda tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha
nne 2012, Profesa. Herne Joseph Mosha kutoka chuo kikuu cha Dar es
salaam, Amesema kuwa serikali inaumuimu wa kuunda tume kuchunguza
matokeo hayo ilikuweza kupata chanzo kimoja ambacho kinazungumzia
chanzo cha matokeo hayo na nini chakufanya baada ya matokeo hayo
mabaya kwani sivyema kuwatumia wanasiasa katika mambo ya kitaalam
“ Sivyema
kuwatumia wanasiasa sana japo nao wanaumuimu, ilikupata mtummoja
ambaye anatoa kiini cha tatizo nilazima tume iundwe kwani serikali
aiwezi kutumia maoni yakila mtu, na pia serikali inayo haki ya kuunda
tume na kwahilo sioni shida” alisema Prof. Herne Mosha
Jinsi
ya kutekeleza mipango ya Elimu ndio bado aijaeleweka, Hakuna ambacho
akijulikani na ninaamini hawatapata kitukipya ndani ya hii tume kwani
tayari vilisha wekwa kwenye tafiti mbalimbali, sera na dira
mbalimbali za elimu zilisema mipango mingi na changamoto nyingi ndani
ya sekta ya Elimu, kushindwa kutekeleza ndio maana bado tunarudi
nyuma, alisema Prof. Herne Mosha
Aidha
Profesa Herne Mosha amesema kuwa kuna haja kwa serikali kuweka Sekta
ya Elimu chini ya Wizara ya Elimu tu nasio ilivyo sasa ambapo sekta
hiyo ikochini ya wizara ya elimu na tamisemi kituambacho kinapunguza
uwajibikaji na kufanya wizara ya elimu kutokuwa na maamuzi yamwisho
hasa kwa walimu namengineyo
“Hakuna
ambaye anaweza kumuwajibisha mwalimu akienda kinyume na mkataba wake,
wala kufuatilia kwa umakini zaidi juu ya mambo fulnai kutokana na
sekta ya Elimu kuwa ndani ya Tamisemi na wakati huohuo iko Wizara ya
Elimu na mafunzo ya ufundi” Hapa napo paangaliwe, alisema Prof.
Herne Mosha
Prof.
Herne alisema kuwa, viashiria vya matokeo mabaya yalianza mwaka 2009
tangu serikali ilipoanza mpango wa maendeleo wa elimu ya secondary
yani SEDEP ambao ulitaka kiasi cha ufaulu kianzie dara la I – III
ambapo ni kwasilimia 32% mpaka asilimia 50% kwani takwimu zinaonyesha
ndipo matokeo ya elimu yalipoanza kushuka. Profesa. Herne Joseph
Mosha alisema
Hatahivyo,
Prof Abdu Ntajuka Hamisi wa Lunga ya Kiswahili UDSM, amesema kuwa
kuundwa kwa tume hiyo nimuhimu kwani tume inatoa matumaini ya kile
walichokibaini kutokana na maoni ya watumbalimbali juu ya matokeo
haya.
“ Tume
italeta matokeo mazuri na yenye njia ya kufanya baada ya hili janga
na kuganga yajayo, kwani nilazima wajue wanaanzia wapi, kwani awawezi
kutoa msaada bila kuwa na data ya nini kifanyike” alisema Prof.
Abdu Hamisi
Prof.
Aliongeza kuwa, kufeli kwa wanafunzi kumanisha kilicho kusudiwa
hakikufanikiwa, ama wanafunzi wamesomeshwa tofauti na mitaala, au
vitabu walivyo someshwa sivyo na pengine watahiniwa awakuwa
waangalifu kulinganisha masomo na mitihani
“Kufeli
kuna maana nyingi sana, pengine kuoanisha matokeo ya kuleta mafanikio
kwenye ufaulu avikufikiwa kwani wameshindwa kufikia walicho kusudia'
Alisema Prof. Abdu Hamisi
Naye
mwalimu wa shule ya sekondari moja ya hapa jijini ambaye hakupenda jina
lake litajwe alisisitiza kuwa serikali itegemee matokeo mabaya mwaka
2013 kwani msingi huu uliopo na ambao umewaangusha hawa waliopita
bado upo na njia ya kutatua kwa sasa imechelewa, Alisema mwalimu huyo
EmoticonEmoticon