Mheshimiwa mama Anna Makinda leo amelaani vikali tukio lililotokea jana jioni wakati wa kujadiliwa kwa hoja ja John Mnyika iliyopelekea Bunge kuahirishwa kabla ya muda husika kufika kuwa ni kinyume cha kanuni za Bunge na kuwa sikweli kwamba kiti cha Spika wa Bunge kinaonea au kupendelea Upande wowote Bungeni hapo
Hoja iliyoleta mzozo ilitolewa na Mhe. John Mnyika kuusiana na swala la maji ambapo Waziri wa Maji Prof. Jumanne Magembe alitaka hoja hiyo iondolewe kwani haikuwa na umuhimu wowote kwa wakati ule sababu iliyopelekea wabunge wa Upinzani kupiga kelele wakiimba CCM mara kadhaa kisha Naibu Spika Job Ndugai kulazimika kuahirisha Bunge
Leo Spika Makinda amewataja wasumbufu kuwa ni John Mnyika na kusisitiza kuwa wengine wanajijua, huku akiwataka Wabunge kueshimu zaidi kanuni za Bunge hilo
HOJA ZA SITISHWA LEO BUNGENI,
LEO Bungeni hakukuwa na hoja yoyote iliyowasilishwa huku baada ya Hoja ya Mhe. Joshua Nassari ikiwekwa kapuni na Spika kwakile alichodai ni utovu wa nidhamu wa viongozi hao maamuzi ambayo yalifanywa na Kamati ya Uongozi wa Bunge nakutangazwa na Spika. Hoja aliyokuwa aiwasilishe Nassari niya Mwenendo wa Baraza la Mtitihani unavyo adhiri Elimu Yetu,
Kusitishwa huko kwa hoja Binafsi kumetokana na wabunge kutokuwa na nidhamu na hivyo kupoteza heshima ya Bunge, Hatahivyo Muwasilisha hoja hiyo Mhe. Nassari alishangwaza na sababu hiyo na kusisitiza kuwa anaye takiwa kusitisha hoja binafsi ni Mbunge mwenyewe
" Kwamujibu wa vufungu vya kanuni ya Bunge, anayetakiwa kusimamisha au kusitisha hija nimtoa hoja mwenyewe, nasio kamati ya Uongozi ni Kamati ya maadili ya Bunge ndio inaweza kuzuia" Alisema Nassari lakini hakupewa nafasi ya kuendelea kujadiliwa Bungeni hapo
MHE. KIGWANGALA AENDELEZA VIOJA VYAKE
Mbunge wa Nzega Mhe. Hamisi Kigwangala leo ameomba nafasi ya kazi ya kutibu baadhi ya wabunge ambao anadai wamepoteza mwelekeo huku akitaka ofisi za Bunge kutoa huduma za kutibu wabunge ambao wanamatatizo
Akiongea Bungeni wakati akitoa pendekezo binafsi kwaajili ya tiba hiyo, Kigwangala nimiongoni mwa wabunge walionekana kutoa maneno ya Kasha kiasi cha kuibua mabishano baina yake na wabunge wengine
Bunge la Feb. 04 2013 Kigwangala aliwsilisha hoja Binafsi ya kutaka serikali kuanzisha mfuko wa kuwasaidia vijana wajasiriamali wanaojikita zaidi kwenye kilimo.
EmoticonEmoticon