Chama
cha Mapinduzi kimepata wajumbe 14 wa kamati kuu ya Halmashauri kuu ya
CCM taifa baada ya kikao cha siku mbili kilichoendeshwa huko mkoani
Dodoma
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Katibu wa halmashauri kuu ya
taifa itikadi na uenezi Bwana Nape Nnauye, anasema halmashauri kuu ya
chama hicho kimeridhia na uteuzi na kufanya uchaguzi wa wajumbe hao
14 wakamati kuu
Aidha
waliochaguliwa na kuibuka kidedea kwa Tanzania Bara ni Ndugu Pindi
Chana, Adam Kimbisa, William Lukuvi, Dr. Emmanuel Nchimbi, Jerry
Slaa, Stephen Wasira na mama Anna Tibaijuka
Kwa
upande wa Tanzania Visiwani – Zanzibar, walioibuka kidedea ni Ndugu
Shamsi Vuai Nahodha, Hussein Mwinyi, Prof. Makame Mbarawa, Dr Salim
Ahmed Salim, Maua Dftari, Samia Suluhu na mama Hadija H Aboud.
Hatahivyo
Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dr. Salim Ahmed
kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 zauteuzi wa
mwenyekiti wa CCM
EmoticonEmoticon