Matokeo
ya kidato cha nne 20012 yametoka hii leo, huku wasichana wakiwa
wameburuzwa sana na wavulana kwa kiwango cha ufaulu. Matokeo hayo
yametangazwa katika wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi jijini Dar
es salaam na waziri wa wizara hiyo Mhe. Shukuru Kawambwa
Octoba
mwaka jana, Jumla ya watahiniwa Laki 126, 847 elfu walifanya mtihani
huo, waliofaulu ni wanafunzi 397,136 huku wasichana wakiwa ni Elfu 46
na161 na wavulana niElfu 80 na 686. idadi inayofanya wavulana kuwajuu
zaidi ya ile ya wasichana
Waziri
amesema, Jumla ya watahiniwa Elfu 23, mia 520 wamefaulu katika daraja
la I-III ambapo katiyao wasichana ni Elfu 7,178 na wavulana ni Elfu
16,342 ambapo wasichana wameburuzwa kawa kiasi kikubwa pia
Shule
10 zilizofanya vizuri ni, St. Francis Girls iliyopo Mbeya, Marian
Boys iliyopo Pwani, Feza Boys iliyopo Dar, Marian Girls iliyopo
Pwani, Rosmini iliyopo Tanga, Canosa iliyopo Dar, Jude Moshono
iliyopo Arusha, St.Marys mazinde juu iliyopo Tanga, Anwarite Girls
iliyopo Kilimanjaro na Kifungilo Girls iliyopo Tanga
Shule
10 zilizofanya vibaya ni Mibuyuni – Lindi, Ndame – Unguja,
Mamndimkongo – Pwani, Chitekete – Mtwara, Maendeleo – Dar es
salaam, Kwamndolwa – Tanga, Ungulu – Morogoro, Kikale – Pwani,
Nkumba – Tanga na Tongoni pia kutoka Tanga
Wanafunzi
24, wamefutiwa mitihani yao kwa sababu ya kuandika matusi katika
script zao, “ Waziri amesema kutokana na kosa hilo baraza la
mitihani limefuta matokeo yao yote kwa mujibu wa kifungu cha 6 (2)a
cha kanuni za mitihani”.
Akitoa
tadhmini ya ufaulu wa mitihani hiyo, Waziri amesema shule zilizo
fanya vibaya zaidi nizile za vijini ambazo hazina kabisa walimi,
miundombinu ni mibovu, hakuna maabara kwaajili ya masomo ya sayansi,
kuna ubungufu mkubwa wavitabu na changamoto mbalimbali
“ Shule
hizi zilizofanya vibaya zinachanga moto nyingi kama nilivyo taja na
Serikali inajitahidi kuzuia changamoto hizo ilikukabiliana nayo, kwa
kuajiri walimu wapya Elfu 13,246 ” Alisema Waziri
MWANAFUNZI BORA HAJAWEKWA HADHARANI
Katika
hali ya kushangaza Wizara haikuweza kumuweka hadharani mwanafunzi
bora wa mwaka 2012 wa kidato cha nne kama inavyo fanya miaka yote,
akijibu swali lililo ulizwa na mwandishi wa habari katika mkutano huo
waziri amesema
“ Sikuweza
kuandaa nimwanafunzi yupi ameshika nafasi ya kwanza kutokana na wengi
kugongana kwa alama, lakini niombe samahani kwa hilo na mtajulishwa
baadae” Alisema waziri
Aidha
aikutolewa tadhmini ya ufaulu kwa mwaka 2011 na hii ya 20012 kwa
kidato cha nne ilikujua kama kiwango kimeshuka au laah. TAKWIMU AMBAZO KILA MWAKA HUTOLEWA
EmoticonEmoticon