Naibu Spika Job Ndugai |
NAIBU Spika Job Ndugai leo amekataa
waziwazi kujadiliwa kwa hoja Binafsi iliyowasilishwa na Mhe. James
Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, hoja
iliyowasilishwa ilikujadili udhaifu uliopo katika sekta ya Elimu
nchini,
Kitukilicho pelekea Wabunge wa upinzani kususia kikao cha
Bunge na kutoka nje ya Bunge
“ Kanuni haijulikani, sikunyingine
jipange vizuri zaidi” Alisema Job Ndungai na kuruhusu hoja nyingine
iwasilishwe huku ya Mbatia ikitupiliwa Mbali
Job Ndugai alisikika mara kadhaa
akimtaka James Mbatia asiingilie mamlaka yake pale alipokuwa akinukuu
baadhi ya vipengele vya kanuni za Bunge ilikusisitiza hoja yake
kueleweka mbele ya Bunge tukufu
“Hapo sasa unangilia mamlaka yangu,
unavaa kiti changu kitu ambacho hakiruhusiwi kisheria” Alisema
naibu spika huku mabishano yakiendelea katiyake na Mhe. mbatia
Hoja ya James Mbatia, ambayo ilikuwa na
Vipengele vitatu ikiwemo ya Kutaka kujua juu ya Marekebisho ya
mitaala ya elimu kwa shule za Sejkondari na Msingi, mbili Mutasari wa
Vitabu vya Shule ya Msingi na vya Sekondari... pamoja na kutokuwepo
kwa mitaala ya Elimu ya elimu
Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi/ Mbunge wa kuteuliwa |
“ Tuweni na Huruma, Imani na Busara
na ungwana utumike katika hili, swala la heli ninalo ongelea hapa sio
shule ambazo watoto wetu wanasomea ni zawatanzania wengine, na
ninaongea “ Above Political Level” Alisema Mbatia kwa uchungu
huku akimwambia spika kuwa hatahukumiwa
Kilio kingine cha Mhe. Mbatia ni
kutowasilishwa kwa Mitaala mpaka sasa kwa wabunge huku serikali
ilitoa ahadi kupitia Waziri shukuru Kawambwa mwaka jana kuwa
angewasilisha mitaala hiyo ilikulidhibitishia Bunge kuwa linalopigiwa
kelele sio kweli
“ Sitoendelea kujadili hoja yangu
mpaka mitaala ya Elimu iwasilishwe Bungeni, ilikudhibitisha uongo
ambao nimeuweka katika hoja yangu” Alisema Mbatia na kukaa chini
Baada ya halihiyo kuwepo ndipo wabunge
wa upande wa Upinzani akiwemo James Mbatia waliondoka Bungeni mmoja
mmoja na kuacha mjadala ukiendelea Bungeni hapo
Hali hiyo ilithibitisha kuwepo kwa
Siasa zaidi nasio uzalendo ni baada ya Mhe. Waziri wa Elimu kusema
kuwa sio kila tafiti inabaini ukweli na kusisitiza kuwa hata hoja ya
Mhe. Mbatia imepitwa na wakati kulingana na muda ambao umetumika
kuandaa tafiti ya hoja yake
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa |
Akiongea mbele ya Bunge Mhe. Shukuru
Kawabwa ameponda juu ya kitabu kilichofanyiwa utafiti na kubaini
mapungufu yaliyopo katika sekta ya elimu nchini tangu 1997
huku
akifafanua mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Elimu nchini
ikiwemo Sera ya Elimu inayotumika hadi hivi sasa
“ Utafiti uliofanywa kwa miaka 17 na
Mheshimiwa Mbati yaweza kuwa kweli wakati mwingine yaweza kuwa ni
uongo kwani sio kila tafiti inapata majibu ya kweli, akitaja maeneo
ambayo yana vipengele vikuu vitatu juu ya mitaala, mutasari wa vitabu
lakini hoja hizo zote” Alisema Mhe Kawambwa
EmoticonEmoticon