Mfumo wetu wa elimu kwa muda mrefu umeonesha udhaifu katika usimamizi, uendeshaji, udhibiti na ugharimiaji tangu Taifa letu lilipo amua kufanya ugatuzi wa madaraka, uliopelekea sekta ya elimu kuendeshwa chini ya wizara tatu tofauti.
Ili kufanya mabadiliko katika Elimu, Tuungane kuitaka serikali kuunda tume ya kitaalamu ya kufanya mapitio makubwa ya mfumo mzima wa elimu inayotolewa tanzania bara ili kwenda sambamba na kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi duniani.
KWA KUWA, Elimu mpaka Kidato cha nne hutolewa bure lakini elimu bora inauzwa.
NA KWA KUWA, imebainika kwa Tanzania ina mfumo wa elimu usiojali usawa kwa kiwango cha juu, mfumo kwa ajili ya makundi mawili, kundi moja la matajiri, na kundi lingine la masikini, na mfumo wa elimu ya shule bora za umma kwa ajili ya watu wa kada ya katikati
NA KWA KUWA, imebainika kwa Tanzania ina mfumo wa elimu usiojali usawa kwa kiwango cha juu, mfumo kwa ajili ya makundi mawili, kundi moja la matajiri, na kundi lingine la masikini, na mfumo wa elimu ya shule bora za umma kwa ajili ya watu wa kada ya katikati
NA KWA KUWA, Asilimia 16 pekee ya bajeti ya sekta ya elimu hutengwa kwa ajili ya kugharimia Maendeleo ya sekta ya elimu wakati jumla ya Taasisi na Wakala 88 ambazo zinatafuna asilimia 84% ya bajeti nzima ya Sekta ya Elimu (bilioni 3,887)
NA KWA KUWA, Mfumo wa elimu hapa nchini unaundwa na kusimamiwa na wizara tatu tofauti ambapo wizara ya elimu pekee kuna zaidi ya taasisi na wakala 88 zilizo chini ya wizara hii ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi, ambazo bajeti yake ya matumizi ya kawaida yanamaliza fedha zote hata kabla hazijaanza kuleta Maendeleo.
NA KWA KUWA, Ukaguzi wa Shule za Msingi na Sekondari nchini hazikaguliwi kwa kiwango cha kuridhisha ambapo asilimia 9.1 ya shule za msingi nchi nzima na asilimia 21.4 ya shule za sekondari zote nchini ndizo hukaguliwa kwa mwaka kutokaka na ugharimiaji hafifu.
NA KWA KUWA, Ugharimiaji hafifu wa sekta ya elimu nchini umedumaza kiwango cha watoto kujifunza darasani kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita ambapo tafiti zinaonesha kuwa “uwezo wa watoto kujifunza kusoma na kuhesabu ni mdogo sana Tanzania” inakadiriwa kuwa asilimia 45% pekee ya watoto wa darasa la 3 wanaweza kusoma kwa ufasaha hadithi ya Kiswahili ya darasa la 2, wakati asilimia 19 pekee ya watoto hao hao wa darasa la 3 wanaweza kusoma kwa ufasaha hadithi ya kingereza ya darasa la 2.
NA KWA KUWA, Kuna pengo kubwa kati ya masikini na matajiri katika mfumo wa elimu ambapo inakadiriwa kuwa watoto 3 kati ya 10 wenye umri kati ya miaka 13 wanatokea katika familia masikini sana (ultra-poor households) ndio walifaulu zoezi la kusoma hadithi za kingereza na kiswahili.
NA KWA KUWA, Utekelezaji wa Sera ya Elimu bure una uwezekano mkubwa wa kuongeza maafa katika ubora wa elimu chini kwa sababu Sera hii imeongeza idadi kubwa ya wanafunzi wanaodahiliwa katika shule za msingi na shule za Sekondari katika shule za umma bila kuwa na ongezeko la bajeti ya uendeshaji, usimamizi na ugharimiaji wake pamoja na kuwa na muunganiko kati ya elimu ya kati na elimu ya chini na elimu ya juu.
NA KWA KUWA, Watoto waishio familia masikini vijijini ndio huathirika zaidi na usimamizi, uendeshaji na ugharimiaji duni wa elimu nchini, ambapo watoto 4 kati ya 10 waliopewa zoezi la kusoma na kuhesabu vijijini ndio waliofaulu, hii maana yake ni kuwa watoto 6 kati ya 10 kutoka vijijini uwezo wao wa kusoma na kuhesabu upo duni sana, ukilinganisha na watoto wa mijini ambao wao 6 kati ya 10 walifaulu zoezi la kusoma na kuandika.
NA KWA KUWA, Mazingira ya watoto kujifunza bado yapo duni sana kutokana na ugharimiaji hafifu, ambapo Utafiti wa Twaweza ulibaini kuwa asilimia 44 pekee ya shule za umma ndizo zinatoa huduma ya chakula shuleni, wakati asilimia 46 pekee ya shule za umma ndizo zina maji safi ya kunywa, na asilimia 31 ya shule zote za umma ndizo zina maktaba wakati kitaifa wanafunzi 30 wanatumia kitabu kimoja kujifunzia.
NA KWA KUWA, Imebainika kuwa Mpango wa Maendeleo wa Miaka 5 katika elimu umepoteza mwelekeo kuhusu ugharimiaji wa sekta ya elimu, ambapo kuna upungufu mkubwa wa ugharimiaji wa elimu ndani ya kipindi cha miaka 5 ijayo, ambapo Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka 5, unapendekeza ugharimiaji wa elimu ya misingi uwe Shilingi Bilioni 1,357 ambazo ni sawa na asilimia 28% ya fedha zote zinazotarajiwa kutengwa kwa miaka yote mitano (Bilioni 4,898.92.)
NA KWA KUWA, Elimu ya Msinig imetengewa bajeti finyu ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2016/17 ambapo Shilingi Bilioni 156.73 zimetengwa kwa ajili ya Maendeleo ya elimu ya Msingi ambazo ni sawa na asilimia 17% ya fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya bajeti ya Maendeleo ya wizara Elimu, Sanyansi, Teknolojia na Ufundi katika mwaka wa fedha 2016/17.
NA KWA KUWA, Mpango wa Maendeleo ya “elimu bure” katika shule za Sekondari umetengewa asilimia 4% pekee ya fedha zote katika miaka mitano ijayo, ambapo hakuna uhalisia katika ugharimiaji wa mpango wa elimu bure nchini kwa shule za sekondari.
NA KWA KUWA, Waalimu wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya madai ya stahiki zao yenye jumla ya shilinigi bilioni 408 na zaidi, wakati motisha na ari yao ikizidi kushuka siku hadi siku.
Kwahiyo basi tuungane kwa pamoja KUSAINI NA KUSHARE ili kwamba serikali ituundie tume ya kitaalamu ya kufanya mapitio makubwa ya mfumo wa elimu inayotolewa tanzania bara ili kwenda sambamba na kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi duniani.
EmoticonEmoticon